Breaking News

DC KILOSA ATAKA DINI ZITUMIKE KUWAUNGANISHA WANANCHI

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, Shaka Hamdu Shaka, akihutubia kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Kigoma Malima katika mashindano ya kuhifadhi Qur'an yaliyofanyika mkoani humo Aprili 6, 2024.

......................................

Na Mwandishi Wetu, Morogoro 

MKUU wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, Shaka Hamdu Shaka, ametaka imani za dini ziendelee kutumika kuwunganisha watanzania, kuhamasisha, amani, umoja na mshikamano.

Aidha, amewasisitiza watanzania kuutumia mwezi mtukufu wa Ramadhan kuwa jukwaa la kuwaelimisha na kuwaunganisha kushikamana na kuleta maelewano.

Shaka ameyasema hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Kigoma Malima alipomwakilisha katika mashindano ya kuhifadhi Qur'an yalioshirikisha washiriki kutoka mikoa ya Morogoro, Pwani na Iringa yaliofanyika katika viwanja vya Msikiti wa Bomani mjini Morogoro. 

Alisema kuwa kila Mtanzania aelewe kuwa taifa  halina dini bali  wananchi  wake ndiyo wenye kufuata imani mbalimbali, hivyo kila mmoja ana fursa ya kuabudu kulingana na Imani yake.

"Kila mtanzania nchi yetu inamtambua ni binadamu anayestahili heshima na haki kwa mujibu wa katiba  yetu. Taifa  letu  katiba yake imempa Uhuru   wa kuabudu bila kuvunja mpaka, Kikitokea chama au kundi  lenye lengo la kuvuruga amani na kupandikiza chuki lilaaniwe na jamii ya watanzania, "alisema  Shaka. 

"Tunahitaji kumshuhudia kila mwananchi akipanda mbegu za amani, umoja na upendo, tunamshukuru Mungu tune Rais Samia mwenye hofu ya Mungu kazi kubwa anaiyoifanya kutunganisha kama Taifa inahitaji kuungwa mkono na kila mmoja wetu ili kuchochea maendeleo endelevu ndani ya nchi," alisema Shaka.

Aidha aliwataka viongozi  wa dini  waendelee na kazi ya kuipika mioyo  ya waumini  wao  huku wakiwahimiza na kuwaeleimisha fadhila na neema za kumuamini Munngu, kuendeleza upendo na kuwajali wenye dini na hata  wasio na dini. 

"Nawahusia muufanye mwezi huu mtukufu  wa Ramadhan uwe jukwaa la uadilifu linalotoa elimu itakayowajengea maarifa  waumini  na wasio na  dini .Viongozo wa dini zote waendelee kuhubiri upendo ndani na nje ya nyumba za ibada . Misikiti na Makanisa yaendelee na kazi ya kuelimisha imani na umoja " Alisema katibu huyo.

Alisema kila muumini  wa dini anahitaji kupata nafasi ya kumuabudu mola wake akiwa katika  mazingira ya amani kwani utulivu , amani na umoja  ukitoweka huwa mwanzo  mitafaruku na vurugu zitakazowanyima  waumini wakose muda wa kufanya ibada zao  kwa utuamo.

Akizungumza kadhi wa Mkoa wa Morogoro, Mohamed Masenga amesifu jitihada za viongozi wa serikali katika kuwaunganisha watanzania jambo ambalo nchi imeendelea kuwa na amani upendo na umoja huku wakishuhudi mipango mbali mbali ya kuletea maendeleo ikifanikiwa. 

Mashindano hayo ya Qur'an ni mwendelezo wa shughuli inayofanyika kila mwaka ambapo imeshirikisha washiriki kutoka mikoa ya Iringa, Morogoro na Pwani na kwa mwaka huu Shaka Hamdu Shaka amekubali kuwa mlezi wa mashindano ambapo washindi walikabidhiwa zawadi mbali mbali. Mmoja wa washiriki wa mashindano hayo akiwajibika kutafuta ushindi.Mkuu wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, Shaka Hamdu Shaka, akitoa zawadi kwa washindi.Zawadi zikiendelea kutolewa.Mdau wa mashindano hayo akionesha furaha yake kwa kumkumbatia Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo.Mashindano hayo yakiendelea.Zawadi zikitolewa.Mshereheshaji wa mashindano hayo akiwajibika. 

No comments