MCHENGERWA AFANYA TENDO LA HURUMA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO RUFIJI ATOA MILIONI 50
................................
Na Mwandishi Wetu, Rufiji
MBUNGE wa Jimbo la Rufiji na Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Mohamed Mchengerwa amefanya tendo kubwa
la huruma baada ya kutimiza ahadi yake kwa kutoa Sh.Milioni 40 kwa wananchi wa
Rufiji walioathirika na mafuriko kwa ajili ya kununulia mbegu za mazao
yaliyosombwa na maji na pia ameongeza Sh. Millioni 10 nakufanya kiasi cha fedha kuwa Sh.Milioni
50 ambazo amemkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele.
“ Mchengerwa ametoa fedha hizo kutoka mfukoni mwake na ni sehemu ya mshahara wake kwa ajili ya kuwafuta machozi wananchi wa Rufiji kufuatia kuathiriwa na mafuriko ni jambo la kizalendo alilolifanya Mungu aendelee kumpa afya njema na maisha marefu kwani ni viongozi wachache wanaofanya hivyo,” alisema mmoja wa wanananchi walioathiriwa na mafuriko hayo ambaye hakupenda kutaja jina lake.
No comments