Breaking News

WANAHABARI SINGIDA WAJERUHIWA TENA, WAKOSA FURSA YA KURIPOTI HABARI ZA KATIBU MKUU WA CCM TAIFA

Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Emmanuel Nchimbi.

.......................................

Na Mwandishi Wetu

WAANDISHI wa Habari Mkoa wa Singida wameendelea kukachwa kwa mara nyingine na kushindwa kupata fursa ya kuripoti habari za ziara ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi aliyoianza Mei 29, 2024.

Baadhi ya waandishi hao wakizungumza kwa nyakati tofauti  wamesema licha ya katibu mkuu huyo wa CCM kufanya ziara yake kwa mara ya kwanza mkoani Singida tangu Halmashauri Kuu ya CCM Taifa chini ya Mwenyekiti wake Rais Samia Suluhu Hassan kumteua kushika nafasi hiyo CCM mkoani hapa imeshindwa kuona umuhimu wa katibu huyo kupewa waandishi wa kutosha ili taarifa zake na maagizo ambayo atayatoa wakati wa ziara hiyo ziweze kuwafikia wananchi wengi wa Singida na Taifa kwa ujumla badala yake wamewaalika waandishi wasiozidi wanne huku wakiwategemea waandishi ambao wapo kwenye msafara wa kiongozi huyo.

“ Sisi waandishi wa Singida ni wazalendo wa nchi pamoja na chama chetu cha CCM hata kama wasingetupa hiyo posho lakini kwa kuzingatia ugeni huu mkubwa wa Katibu wa CCM Taifa Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi Mwanadiplomasia mbobezi tulikuwa tupo tayari kwenda kuandika habari za ziara yake wao wangetutafutia usafiri ingetosha kuliko kukosa kabisa fursa hiyo muhimu ya kuandika habari za kiongozi wetu huyu ambaye amefika mkoani kwetu kwa mara ya kwanza.” alisema mmoja wa waandishi hao.

Tukio hilo la kujeruhiwa kwa waandishi hao lina kuja baada ya siku chache kupita tangu yatolewe malalamiko mengine wakidai kutoshirikishwa kuandika habari za ofisi ya mkoa huo ambapo pia CCM mkoani humo nao wakilalamikia kuwa na kikundi chao cha waandishi wanaoandika habari zao kila wanapo kuwa na ziara za kikazi na hata wanapofika viongozi mbalimbali wa chama hicho kitaifa bila ya kuweka utaratibu wa kubadilishana licha ya mkoa huo kuwa na waandishi wa habari zaidi ya 35.

Hata hivyo mmoja wa kiongozi wa CCM mkoani humo ambaye jina lake tunalo akizungumza na mwandishi wetu alisema kuwa juzi asubuhi kupitia Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Singida (Singida Press Club), Elisante John walitoa mualiko wa waandishi wa habari zaidi ya 12 kwa ajili ya kushiriki ziara hiyo lakini ilipofika jioni waliamua kuwaacha wote na kuwachukua wanne tu kwa kuwa walikuwa hawana fedha za kuwapa kama posho iwapo kama wangechukuliwa wote.Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Martha Mlata.

Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Lucy Boniface

Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Mkoa wa Singida, Elphace Lwanji
 

No comments