ANAYETAKA KUNIKERA ANIKANYAGIE UCHUMI WANGU - RAIS SAMIA
.....................................
KATIKA hafla ya kupokea gawio na
michango kutoka mashirika na Taasisi za umma, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewaeleza viongozi mbalimbali
walioshiriki katika hafla hiyo na kutoa ujumbe kwa Watanzania ya kuwa mtu atakayetaka
kukanyaga uchumi wa Taifa letu la Tanzania moja kwa moja mtu huyo atakuwa
sehemu ya kumkera yeye kama kiongozi mkuu wa Taifa hili.
Rais Samia amesema wazi ikiwa ni katika kuonesha dhamira yake ya dhati ya
kutaka kuona mageuzi makubwa ya kukua kiuchumi kwa Taifa letu kwa kuzingatia
utekelezaji wa ilani uchaguzi ya CCM (2020/2025) , sera na miongozo katika
Taifa.
Aidha, Rais Samia amesema kuwa katika hatua za kupata mageuzi ya kiuchumi
wapo baadhi ya watu watakaokanyagwa ambao wataonesha kutokwenda mbele.
" Katika mageuzi haya tutawakanyaga watu wengi sana wale ambao
hawataki kwenda mbele na ndio watakaopiga kelele nyingi sana..sasa ndugu yangu
wewe, mwanangu wewe uliye kwenye shirika ambaye hutaki kukanyagiwa nguru wako
nenda kachape kazi.. " alisema Rais Samia.
" ..leteni mageuzi, chapeni kazi kwenye mashirika ili tuone tija ikionekana basi hatutakanyaga nguru wako lakini kama utataka kunikanyagia mimi nguru wangu wa uchumi..aaah na mimi nitamkanyaga wako...tufanye kazi ili tulete tija kwa Taifa, makelele tusiyasikilize, tupande mti kisha tukishuka tutawauliza mnasemaje.. " alisema Rais Samia.
No comments