Breaking News

MFANYABIASHARA HAIDARY GULAMALI MDAU ANAYEKISAIDIA CCM NA JAMII

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa akipeana mkono na Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Kiwanda cha Magodoro Dodoma Asilia, Haidary Gulamali, alipokuwa akimkabidhi magodoro 200 yenye thamani ya Sh. Milioni 10 ukiwa ni msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika baada ya Waziri Mkuu kutembelea kiwanda hicho Oktoba 2, 2016. Kushoto ni aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama.

............................

Na Dotto Mwaibale

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kitajengwa na wana chama wenyewe, jumuiya zake pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo ambao ni waadilifu na wazalendo wa ukweli.

Mei 31, 2024 Katibu Mkuu wa chama hicho Taifa Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi na wajumbe wake alimaliza ziara yake ya kikazi mkoani Singida akiendelea na ziara hiyo katika mikoa ya Manyara, Arusha na kumalizia Mkoa wa Tanga.

Akiwa Mkoa wa Singida moja ya jambo kubwa alilolifanya ambalo lina kwenda kuacha alama ni harambee kubwa aliyoifanya ya kupata fedha za kumalizia ujenzi wa jengo la CCM Mkoa ambalo ujenzi wake ulianzishwa mwaka 1985 na Baba yake Katibu huyo ambaye alikuwa ni Katibu wa chama hicho Mkoa wa Singida na Mkuu wa Mkoa huo Hayati Mzee John Nchimbi chini ya Mwenyekiti wa kwanza wa CCM mkoa huo,  Mzee Timothy Zakaria  Kingu ambao watabaki kuwa tunu ya Mkoa wa Singida na Tanzania kwa ujumla.

Harambee hiyo ya aina yake iliyofanyika Ukumbi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida sanjari na hafla ya chakula cha usiku iliyokuwa mahususi kwa katibu huyo na ujumbe wake iliyoandaliwa na CCM mkoani hapa na kuwa ya mafanikio makubwa kwani jumla ya Sh. Milioni 200 zilipatikana baada ya wadau, viongozi wa Serikali, wabunge na wana CCM wenyewe kujitokeza kwa wingi kushiriki.

Miongoni mwa wadau wa chama hicho ambaye alionekana kuing'arisha harambe hiyo na kuwa kinara kwa upande wa makada wa kawaida na wadau wengine ni Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Kiwanda cha Magodoro Dodoma Asili, ambaye alichangia Sh.Milioni 20 na kuvunja rekodi ya wote waliochangia ukiondoa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Singida ambayo ilitoa Sh.Milioni 20, kamati ya siasa  mkoa Sh. Milioni 20 huku Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida kupitia  mkuu wa Mkoa huo Halima Dendego  wakiahidi kutoa Sh.Milioni 90 ambayo ndio taasisi pekee ya Serikali iliyotoa  fedha nyingi,

Wengine waliochangia katika harambee hiyo ni kada wa chama hicho, Lazaro Nyalandu ambaye alitoa Sh.Milioni 19 ambapo kwa upande wa Wabunge wa Mkoa wa Singida Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Miraji Mtaturu aliongoza kwa kutoa Sh. Milioni 10 akifuatiwa na Mbunge wa Viti Maalumu mkoani humo, Aysharose Mattembe ambaye alitoa Sh. Milioni 5.

Gulamali amekuwa mdau mkubwa wa maendeleo ndani ya chama hicho na kwa jamii hasa pale yanapotokea matukio yanayohitaji msaada kwa waathirika kama matetemeko na  mengine yanayofanana na hayo kama kusaidia ujenzi wa shule kwa kutoa vifaa vya ujenzi..

Kutokana uzalendo wake huo mkubwa kwa chama na nchi Gulamali amekuwa akiyagusa maisha ya watanzania wengi katika maeneo mbalimbali nchini licha ya yeye kuwa mkazi wa Dodoma.

Mwaka 2016 lilipotokea tetemeko la ardhi mkoani Kagera kupitia kiwanda hicho cha magodoro, Gulamali alitoa magodoro 200 yenye thamani ya Sh.Milioni 10  na kumkabidhi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa ajili ya kuwasaidia waathirika.

Ikiwa hiyo haitoshi kwa nyakati tofauti aliwahi kumkabidhi magodoro 200 aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge. ikiwa ni mchango wake kwa ajili ya hospitali za mkoa huo. 

Halikadharika tukio la namna hiyo alilifanya kwa kutoa magodoro 1, 000 aliyomkabidhi aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa ajili ya Hospitali za mkoa huo.

Aidha tukio jingine kama hilo mfanyabiashara huyo alilifanya kufuatia maafa yaliyotokea mkoani Dodoma ambapo alichangia magodoro 200 ambayo alimkabidhi Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde. 

Afisa Mtendaji huyo Mkuu (CEO) wa Kiwanda cha Magodoro cha Dodoma Asili, Haidary Gulamali katika kusaidia jamii kiafya kwa ufadhili wake alifanikiwa kuwaleta nchini madaktari bingwa kutoka India kwa ajili ya kusaidia upasuaji wa moyo na huduma mbalimbali za afya. 

Aidha, Gulamali aliwasaidia wanawake (UWT) 1,500 kupima afya zao na saratani ambapo huduma hiyo waliipata bure pamoja na ghrama za upasuaji kwa waliogundulika kuwa na changamoto. 

Madaktari hao bingwa kutoka India waliletwa kwa ufadhili wa mfanyabiashara huyo Haidary Gulamali kwa ajili ya kufanya upasuaji wa moyo na kutoa huduma mbali mbali za afya kwa ufadhili wake huduma zilizofanyika Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma na Bugando Mwanza.

Aliyekuwa Mkuu wa  Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipokea magodoro 1,000 kwa ajili ya Hospitali za mkoa huo.


Aliyekuwa Mkuu wa  Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge (mwenye mvi). akipokea magodoro 200 kwa ajili ya Hospitali za mkoa huo.

Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akipokea magodoro 200 kwa ajili ya waathirika wa maafa yaliyotokea Dodoma.

Ndg Haidary Gulamali akiwa na baadhi ya  wakina mama kati 1,500 ambao walipata huduma bure za uchunguzi wa saratani na magonjwa mengine kwa ufadhili wake.

Ndg Haidary Gulamali akiwa na baadhi ya  wakina mama hao.
Wakina mama wakisubiri kupata huduma baada ya kufadhiwa na Haidary Gulamali.
Ndugu Haidary Gulamali akikabidhi saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule.
Picha ya pamoja baada ya makabidhiano ya saruji.
Ndugu Haidery Gulamali akitoa msaada kwa mmoja wa wanafunzi.
Haidary Gulamali akitoa msaada wa viti.
Viti na vyarahani vilivyotolewa na mdau wa maendeleo Haidary Gulamali.
Ndugu Gulamali akitoa msaada wa viti na vyerehani kwa wana CCM.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Kiwanda cha Magodoro Dodoma Asili wakati alipotembelea kiwanda hicho mwaka 2016 ambapo pia alikabidhiwa magodoro 200 kwa ajili ya waathiri wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoa wa Kagera.

(Picha zote kwa hisani ya Maktaba ya Haidary Gulamali) 

No comments