Breaking News

ZANZIBAR KUSHIRIKIANA NA CHINA KATIKA UTAFITI NA TAALUMA ZA AFYA

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

WAZIRI wa Afya Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui amesema watashirikiana na Chuo Kikuu cha Fudan Medical collage cha Shanghai cha nchini China katika masula mazima ya tafiti na taaluma za afya.

Waziri Mazrui ameyaeleza hayo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka chuo kikuu cha Fudan Medical collage ambao umefika hapa nchini kuetembelea sehemu mbali mbali katika sekta ya Afya.

Amesema hivi sasa Chuo na Wizara ya Afya wanamkataba wa kuimarisha masuala mazima ya tafiti kupitia Taasisi ya utafiti ZAHRI Binguni na katika kuendelea mbele zaidi, watasaini mkataba mwengine mwezi wa Novemba mwaka huu ya mashirikiano baina Wizara ya Afya na Chuo kikuu hicho.

Amefahamisha kuwa kutokana na chuo hicho kuwa na hospitali zaidi ya 14 ambazo zinaendeshwa na chuo hicho na wanawataalamu wa kila fani Wizara ya Afya itahakikisha wanapata fursa za kuwapeleka wafanyakazi kusoma zaidi nchini humo katika kada mbali mbali.

Alifahamisha kuwa kuja kwa ujumbe utasaidia katika kuongeza mambo mbali mbali ya kuimarisha sekta afya hapa nchini ambayo yatahusika katika mkataba huo.

Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha Fudan Medical collage cha Shanghai nchini china Zhenghoug Yuan amesema lengo la kuja hapa nchini ni kuimarisha ushirikino uliopo baina ya Zanzibar na China sambamba na kuimarisha masula ya tatiti za kifya na masomo kwa wafanyakazi.

Zanzibar na China inamashirikiano makubwa tangu mwaka 1964 na inasadia katika sekta mbali mbali ikiwemo Afya kwa kuwapatia madaktari wa kutoa huduma Unguja na Pemba.
Picha ya pamoja
 

No comments