DKT. HUSSEIN ALI MWINYI RAIS WA ZANZIBAR ANAYEFANYA MAPINDUZI MAKUBWA YA KIUCHUMI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi alipokuwa akivuta pazia na Balozi Mdogo
wa Jamhuri ya Watu wa China anayefanyia kazi zake Zanzibar . Zhang Ming kuashiria uzinduzi wa nyumba hizo (kushoto kwa Rais), ni Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Nassor Ahmed Mazrui
na Naibu Waziri wa Afya Mhe. Hassan Khamis Hafidh
.....................................................
Imeandaliwa na Dotto Mwaibale, (0754-362990)
UONGOZI ni dhana
au taaluma inayompa mhusika madaraka na uwezo wa kuwawezesha wale wanaongozwa naye kuunganisha nguvu, stadi na
vipaji vyao na kuvitumia ili kufikia malengo yao
mbalimbali.
Duniani kumekuwa na aina mbalimbali za viongozi kama vile Wafalme, Marais, Mawaziri, Watemi, Machifu, Wakurugenzi, Viongozi wa dini na wengine wote huku baadhi yao wakipata nafasi hizo kwa
kurithi, kwa kuchaguliwa, kuteuliwa na
mamlaka za juu zaidi, kupata uongozi wa kimila na kupata wadhifa huo kwa njia ya kidemokrasia.
Mara nyingi uongozi wa kidemokrasia ni ule wa kushirikisha watu
katika kufanya maamuzi na utekelezaji wake na mara nyingi viongozi wa aina hiyo hulenga kukidhi
mahitaji ya walengwa.
Viongozi wanaochaguliwa mara nyingi huwa wanapewa muda wa
kuongoza, na wale wanaojiteua hujipatia wao wenyewe muda wa kuongoza au hata
hapo watakapoamua kuachia madaraka.
Baadhi
ya sifa za kiongozi bora anatakiwa kuwa na ufahamu mkubwa juu ya taasisi anayoiongoza, malengo yake, mazingira na matatizo yake,awe mwaminifu. kila taasisi inalenga kufikia shabaha fulani. Hivyo ni wajibu wa kiongozi kuwaongoza wanataasisi ili wafikie
malengo yao.
Sifa
nyingine ya kiongozi ni lazima aweze
kubuni mikakati na mbinu zitakazoiwezesha taasisi anayoongoza kufikia
malengo yake, Awe na maadili mema. ni lazima akubalike katika jamii na taasisi anayoiongoza. Na ili akubalike
hana budi kuzingatia maadili ya msingi ya jamii na taasisi yake kwani mtu
muongo, mlevi, mvivu, asiye mwaminifu na mambo mengine yanayofafanana na hayo hawezi
kuwa kiongozi mzuri.
Aidha
sifa nyingine ya kiongozi anatakiwa awe mcha Mungu, akubalike na watu
anaowaongoza na awe
anaongoza
watu katika misingi bora ya uongozi bila kujali jinsia, rangi, dini,
cheo, wala kabila na
kuwathamini watu wa makundi yote, awe anakubali kushauriwa ua kupokea ushauri
kutoka kwa wengine.
Awe na uwezo wa kujifunza kutoka kwa watu wengine waliofanikiwa,
awe na mawazo ya mbele ya kuona tatizo na kuonyesha baadhi ya njia za
kulitatua, pamoja na kuona fursa.
Leo napenda kumzungumzia Dkt. Hussein Ali Mwinyi Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliyepata madaraka hayo kwa njia ya
demokrasia na kukidhi vigezo na sifa za kuwa kiongozi.
Dkt. Mwinyi tangu achaguliwe kushika nafasi hiyo amekuja na mapinduzi makubwa ya maendeleo katika sekta ya Elimu, Afya, Kilimo, Barabara, Umeme na kuinua uchumi wa Wanzibar kwa kuboresha mambo kadhaa wa kadhaa huku sera yake kubwa ikiwa yajayo yanafurahisha.
Nitakuwa mchoyo wa fadhira iwapo sitawataja marais waliowahi kuongoza Zanzibar kwani nao kwa namna moja au nyingine walifanya maendeleo
makubwa na walipokuwa wameishia ndipo alipoanzia Dkt. Hussein Ali Mwinyi Rais wa Nane wa
Zanzibar kuendeleza jitihada hizo za kuipeleka mbele Zanzibar kiuchumi.
Angalia orodha ya Marais hao hapa chini
Jina |
Muda wa Utawala |
||
12 Januari 1964 |
7 Aprili 1972 |
||
11 Aprili 1972 |
30 Januari 1984 |
||
30 Januari 1984 |
24 Oktoba 1985 |
||
24 Oktoba 1985 |
25 Oktoba 1990 |
||
Dkt. Salmin Amour |
25 Oktoba 1990 |
8 Novemba 2000 |
|
8 Novemba 2000 |
2010 |
||
3 Novemba 2010 |
2020 |
||
3 Novemba 2020 |
|
Kazi anayoifanya Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, tangu ameingia madaraka sasa akiwa na
miaka minne hakuna mtu ambaye atasema hajaiona hivyo anapaswa kuungwa mkono
na wapenda maendeleo wote.
Licha ya kuwepo usemi uliozoeleka miongoni mwa jamii kuwa yajayo
yanafurahisha mimi nataka kuubadilisha na kuwaambia
Wazanzibar kuwa yajayo sasa yametimia hivyo wasubiri makubwa zaidi kupitia Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi aliyoianzisha Dkt. Mwinyi yenye lengo la kuwafikisha katika uchumi wa juu kutokana na rasilimali walizonazo zitokanazo na bahari.
Wizara
hiyo ambayo imeanzishwa rasmi mwezi wa Novemba 2020 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, Dkt Hussein Ali Mwinyi, kwa uwezo aliopewa na Kifungu namba 41 (2)
cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Lengo
Kuu la Wizara hiyo ni kusimamia utekelezaji wa kasi na endelevu wa fursa
zilizopo na vipaumbele vyake vya uchumi unaotegemea rasilmali za bahari au
Uchumi wa Buluu ili kuijenga Zanzibar mpya yenye uchumi wa kisasa.
Wizara inatekeleza majukumu yake kwa
kuzingatia matumizi na usimamizi endelevu wa bahari na ukanda wa pwani pamoja
na kusimamia, kuratibu na kuimarisha fursa za uwezeshaji na uwekezaji katika
sekta za uvuvi, mazao ya baharini, kilimo cha mwani na utafutaji na uchimbaji
wa mafuta na gesi asilia.
Dira
ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050 “Vision 2050” imeiweka sekta ya Uchumi wa
Buluu kuwa sekta kuu ya kukuza uchumi wa Zanzibar ili kuitoa Zanzibar katika
umasikini na kuifikisha kuwa nchi yenye kipato cha kati cha hali ya juu (Upper
Middle Income).
Mpango
wa uimarishaji wa sekta ya Uchumi wa Buluu unaenda sambamba na utekelezaji wa
Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 – 2025, Mpango wa Maendeleo wa
Zanzibar (ZADEP) wa Mwaka 2021 – 2026, Sera na Mikakati ya Uchumi wa Buluu,
Sera ya Uvuvi na Mazao ya Baharini, Sera ya Mafuta na Gesi, pamoja na mipango
jumuishi na shirikishi ya sera nyingine mbali mbali za kitaifa zinazohusiana na
usimamizi wa bahari na Uchumi wa Buluu.
Halikadhalika,
katika utekelezaji wa maazimio na mikataba ya kimataifa, Wizara ya Uchumi wa
Buluu na Uvuvi ina jukumu la kuhakikisha utekelezaji na ukondoishaji wa
mikataba mbali mbali ya kimataifa yanyohusiana na usimamizi wa bahari na Uchumi
wa Buluu hususan kwa Zanzibar. Lengo Namba 14 la ‘Malengo ya Maendeleo Endelevu
(SDG 14) la Umoja a Mataifa linalohusiana na Usimamizi na Maendeleo Endelevu ya
Bahari, Lengo Nambari 6 la Agenda ya Umoja wa Afrika ya Mwaka 2063 (Agenda
2063), pamoja na mikataba na itifaki mbali mbali za kikanda na kimataifa na
kikanda inayoongoza na kuhimiza uimarishaji wa Uchumi wa Buluu.
Utalii
wa Zanzibar ni utalii wa bahari. Ni utalii unaotegemea uhai na afya ya bahari
na rasilmali zake. Hivyo Utalii Endelevu ni ule unaojali hifadhi za maeneo ya
bahari, bioanuwai ya bahari, usafi na mazingira safi ya fukwe na bahari zake.
Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi inapigania sana Utalii Endelevu wa Zanzibar
unaojali mazingira ya bahari pamoja na mila na desturi za watu wa Zanzibar.
Serikali itahakikisha uhifadhi wa mila, desturi na tamaduni za nchi, chini za
kaulimbiu ya “Utalii Endelevu kwa Wote”, unaozingatia ustawi wa jamii, utalii
wa ndani wa unaotunza mazingira na usimamizi jumuishi wa ukanda wa pwani.
Vipaumbele
vikuu vya Utalii Endelevu kwa Zanzibar ni pamoja na:
•
Kukuza matamasha ya kimila na ya kitamaduni na mila za kienyeji katika Uchumi
wa Buluu.
• Kuongeza uwelewa kwa watalii juu ya mila na desturi katika maeneo ya ukanda
wa pwani.
• Kukuza utalii jumuishi unaozingatia uwekezaji na haki za jamii.
• Kukuza uelewa wa utunzaji wa mazingira na jamii kusimamia rasilimali zao ili
kuhakikisha maendeleo endelevu na kuvilinda viumbe vilivyo hatarini kutoweka.
• Kukuza usimamizi shirikishi wa ulinzi na usalama katika maeneo ya kitalii
kupitia Mpango Maalumu wa Matumizi ya Bahari.
• Kuimarisha mifumo ya kuifanya Zanzibar iendelee kuwa kivutio kikuu cha
utalii; na kutekeleza mpango mkuu wa kuijengea uwezo sekta ya utalii Zanzibar.
Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar inaendelea na mchakato wa utafiti, utafutaji na uchimbaji
wa mauta na gesi hasa katika ameneo ya bahari Zanzibar. Lakini, licha ya kuwepo
kwa taasisi maalumu zinazohusika na utafutaji wa mkondo wa juu wa Mafuta na
Gesi Asilia bado kuna changamoto mbali mbali katika kuharakisha upatikanaji wa
matunda ya Sekta hii.
Ndio
maana Serikali kupitia Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi itaendelea kuhakikisha
uwepo wa usimamizi bora wa shughuli za mafuta na gesi asilia na kuongeza uwezo
wa taasisi zilizopo zinazoshughulikia udhibiti na utafutaji wa mafuta na gesi
asilia, ikiwa ni pamoja na kuiongezea Kampuni ya Mafuta ya Zanzibar jukumu la
kufanya biashara ya mafuta na gesi asilia kwa mkondo wa chini.
Vipaumbele
vya Sekta hii ya Mafuta na Gesi ni pamoja na:
•
Kuongeza uwezo wa kitaasisi katika kusimamia na kukuza sekta ya mafuta na gesi
asilia.
• Kuipatia Kampuni ya Mafuta ya Zanzibar jukumu la kufanya biashara ya mafuta
na gesi asilia kwa mkondo wa
chini.
• Kuimarisha uwezo wa taasisi za mafuta na gesi asilia kwa kufanya marekebisho
ya kisera na kisheria.
• Kuandaa mikakati ya mawasiliano bora juu ya maendeleo ya utafutaji na
uchimbaji mafuta na gesi asilia.
• Kufanya na kusambaza tafiti za kimkakati za tathmini ya athari za Mazingira
zinazohusu maendeleo ya mafuta na gesi asilia.
• Kuendeleza mchakato wa mashauriano na jamii kuhusu maendeleo ya mafuta na
gesi asilia.
• Kujenga uwezo wa kiutendaji na mbinu za uwezeshaji kwa ajili ya kuwanufaisha
wazawa.
• Kutenga eneo lililo salama kwa ajili ya ujenzi wa Hifadhi ya Taifa ya Takwimu
za mafuta na gesi asilia.
• Kujenga uwezo wa usalama na uhifadhi wa takwimu kwa ajili ya Hifadhi ya Taifa
ya Takwimu za mafuta na gesi asilia.
• Kuanzisha taasisi mahiri yenye mfumo imara utakaohakikisha usimamizi bora wa
mapato ya mafuta na gesi asilia.
• Kuanzisha mfumo wenye uwazi wa ukusanyaji wa mapato ukaosimamia maamuzi na
matumizi ya mapato ya mafuta na gesi
asilia kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi
• Kuunda programu za uhamasishaji wa umma juu ya usimamizi wa mapato ya mafuta
na gesi asilia.
Sekta ya Uvuvi na
Mazao ya Baharini
Sekta ya Uvuvi ni mojawapo ya nguzo kuu za Uchumi wa Buluu Zanzibar na imeendelea kuwa sekta muhimu sana katika kupunguza umaskini na kuleta maisha bora kwa jamii kupitia uzalishaji wa ajira.
• Sekta hii inaajiri watu wanaokisiwa kufikia 78,859 ambao ni sawa na asilimia
8.5 ya nguvu kazi yote ya Zanzibar.
Shughuli nyingi za uvuvi hapa Zanzibar ni za uvuvi mdogo ambazo hufanyika katika maji ya kina kidogo cha bahari na kwa kutumia njia za asili. Hata hivyo, mahitaji ya bidhaa za samaki kitaifa na kimataifa yanaongezeka.
• Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia programu zake mbali mbali za
maendeleo ikiwemo utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi inatekeleza
programu ya uwezeshaji wa wavuvi wadogo wadogo kupitia Mradi wa Ahweni wa
UVIKO19 kwa kuwapatia elimu, nyenzo, boti za kisasa na vifaa vya kuvulia Samaki
wananchi wote Unguja na Pemba.
Programu hii inakwenda sambamba na Programu
mbali mbali za wadau wa maendeleo katika Sekta ya Uvuvi ikiwemo UNDP, UN Women,
IFAD, Benki ya Dunia, Umoja wa Ulaya, Ufaransa, JICA, KOICA, n.k.
• Halikadhalika, eneo la Ukanda wa Kiuchumi Baharini lina uwezo mkubwa wa kuvutia uwekezaji wa uvuvi kimataifa na hivyo kutoa fursa kubwa kwa wawekezaji wazawa na wa kigeni kwa kuzingatia mabadiliko ya nchi kuelekea Uvuvi wa viwanda.
• Sekta ya ufugaji wa viumbe maji Zanzibar inajumuisha ufugaji wa samaki,
matango bahari, kaa tope, pweza, chaza, kombe na ukulima wa mwani. Maeneo
muhimu ya kuendeleza ufugaji wa viumbe maji ni pamoja na mabwawa, vizimba, na
maeneo yenye kujaa maji na kupwa. Sekta hii imeendelea kukuwa kwa kasi kubwa na
kuleta mageuzi makubwa ya fursa za Uchumi wa Buluu hapa Zanzibar.
Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi kwa hivi sasa inatekeleza vipaumbele mbali mbali ikiwemo:
•
Kuwawezesha wananchi kitaaluma na kimtaji katika uvuvi na mazao ya baharini.
• Uongezaji wa thamani , uhimilivu na upunguzaji wa athari za mabadiliko ya
tabianchi pamoja na
kuboresha hali za maisha ya jamii ya watu wa mwambao.
• Kukuza uwekezaji katika miundombinu inayohusiana na bahari kuu na kusaidia
ujasiriamali kwenye eneo tengefu la uwekezaji
kiuchumi baharini.
• Kutumia teknolojia, miundombinu na ujuzi katika kupunguza upotevu wa mazao ya
baharini baada ya mavuno.
Mbali
ya kazi hiyo kubwa aliyoifanya ya kuanzisha wizara hiyo baadhi ya kazi nyingine
chache kati ya nyingi alizozifanya Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi ni
ujenzi wa miundombinu ya barabara, Ujenzi wa Hospitali katika Wilaya zote.
Katika
uboreshaji wa huduma za afya Rais wa Zanzibar Dkt. Mwinyi kupitia waziri wake
wa Afya Nassor Mazrui aliagiza huduma hizo ziiendelea kutolewa bure kwa
vipimo vyote vikubwa na vidogo ambapo alitangaza Hospitali zote Zanzibar
zilizojengwa na Rais mwinyi sasa zitasimamiwa na sekta binafsi kwenye
uwendeshaji ili kuwa na huduma za kimataifa.
Alisema Wizara ya Afya iliingia makubaliano maalum ya Uendeshaji
na usimamizi na sekta binafsi ikiwemo EHN na TCL na kusisitiza kuwa wizara hiyo
haikubinafsisha bali ni kuongeza ufanisi wa hospitali hizo zikiwemo za wilaya
na za mikoa ili wananchi wapate huduma bora.
Katika kuimarisha Usimamizi
na Utawala wa Kodi Rais Dkt. Mwinyi
ameanzisha mfumo wa Uunganishaji wa
Mifumo ya Forodha (TANCIS), Usajili wa Gari (MVLRS) na Mfumo wa VFMS ambao
unajulikana kama mfumo wa TANCIS ambao tayari umeunganishwa na mfumo wa usajili
wa magari (Motor Vehicles Licensing and Registration System - MVLRS) na pia
unaimarishwa zaidi ili kudhibiti usajili wa gari zinazoingia nchini, na kupata
takwimu sahihi za Ankara za Kodi (input tax) kwa waingizaji (importer) pamoja
na kufuatilia mwenendo wa walipakodi na kuanza kukusanya kodi ya mapato kwa
Kampuni za Kigeni za Usafirishaji (non - resident person) ambapo utekelezaji wa
hatua hiyo umeanza rasmi Julai, 2022 na
hadi kufikia Machi, 2023 Sh. Milioni 37 zilikuwa zimekusanywa kutokana na
kampuni za kigeni za usafirishaji wa abiria na mizigo.
Kazi nyingine iliyofanyika ni
upatikanaji wa maji safi na salama ambayo ni sehemu ya haki ya msingi ya
binadamu na kuwa Sekta ya maji inakumbwa
na ongezeko la mahitaji ya huduma hiyo kunakochochewa na ongezeko la idadi ya
watu, kukua kwa miji pamoja na kuimarika kwa shughuli za kiuchumi na kijamii
ikiwemo uwekezaji na utalii, mabadiliko ya tabianchi, uvamizi wa vianzio vya maji,
uchakavu wa miundombinu ya maji na mwitikio mdogo wa wananchi kuchangia huduma
ya maji, vyote hivyo vinaipa changamoto kubwa sekta ya maji.
Serikali itaendelea na mikakati ili
kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi Mijini na
Vijijini inafikia zaidi ya asilimia 85 ifikapo mwaka 2025.
Serikali inaendea kutekeleza miradi ya maji hadi
kufikia mwezi Machi, 2023 hali ya uzalishaji maji nchini iliendelea kuimarika
ambapo kwa ujumla wastani wa uzalishaji wa maji umefikia asilimia 67 kwa Unguja
na Pemba ikilinganishwa na asilimia 56 iliyofikiwa mwezi Machi, 2022.
Aidha, mahitaji ya maji Zanzibar yameendelea
kukua ambapo hadi kufikia mwezi Machi, 2023 mahitaji ya maji yamefikia lita
240,465,120 kwa siku na uzalishaji ni lita 146,926,338 kwa siku hivyo kupelekea
kuwa na upungufu wa lita 93,538,782 kwa siku.
Kukamilika kwa miradi ya maji ambayo inaendelea kutekelezwa katika kipindi hichi kutanufaisha wanawake takriban 355,523 na hivyo,kuwezesha wanawake hawa kujishughulisha na shughuli nyingine za kiuchumi na uzalishaji zaidi katika muda ule ambao wanaoutumia katika kutafuta maji.
-
Kazi nyingine kubwa iliyofanyika katika Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Serikali inaendelea na Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 - 2025 ili kufikia dhamira zilizowekwa kupitia Dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2050.
Uwezeshaji wananchi kiuchumi ni miongoni mwa mikakati mahsusi inayotekelezwa kwa lengo la kuinua kipato cha mwananchi, mjasiriamali na mfanyabiashara kwa kuwawezesha kwa kuwapa mafunzo, mikopo na masoko ya bidhaa zinazozalishwa na Wajasiriamali. Hadi kufikia Machi 2023, Serikali imefanikiwa kutoa mikopo 2,177 yenye thamani ya Sh. 14.03 Bilioni ambapo Unguja zilitolewa Sh. Bilioni 9.34 na Pemba Sh. Bilioni 4.69.
Katika
shughuli zinazotoa Huduma Ndogo Ndogo za Kifedha hadi kufikia Machi, 2023 jumla ya vyama vya
ushirika vilivyosajiliwa ni 1,822 (Unguja 1,036; Pemba 786), SACCOS 2 na vyama
vya uzalishaji na utoaji wa huduma 1,820.
Aidha,
hadi kufikia Machi, 2023 jumla ya taasisi sita (6) zimepatiwa ruhusa ya
kufanyakazi za huduma ndogo ndogo za kifedha Zanzibar ambapo lengo ni kusajili
vyama 300 (Unguja; 200, Pemba 100) na kuwa utekelezaji wa zoezi hili
umeongezeka zaidi ya mara mbili ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana
ambapo Idara ilisajili jumla ya vyama 914.
Aidha kazi nyingine kubwa iliyofanywa na Rais wa Zanzibar ni ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.
Katika kuongeza maboresho ya sekta ya Elimu,Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar wamepanga kuimarisha uongozi na usimamizi wa elimu katika ngazi zote ikiwemo Skuli, Wilaya, Mkoa na Wizara.
Hayo yalibainishwa na Waziri wa Elimu Zanzibar Lela Muhamed Mussa wakati
akiwasilisha Bajeti ya Wizara hiyo katika Baraza la Wakilishi Zanzibar.
Alisema wataimarisha mfumo wa tathmini ya maendeleo ya elimu ya wanafunzi katika
ngazi zote za elimu na kupandisha ufaulu wao kuimarisha miundonmbinu ya Elimu
Aidha alisema katika kujenga madarasa 1500 kupitia ujenzi wa Skuli za Ghorofa,
Skuli za Chini na kukamilisha madarasa yaliyoanzishwa na
wananchi, kwa Unguja na Pemba, nyumba 20 za walimu, Ofisi ya Wizara, Ofisi 4 za
Elimu Wilaya, vyoo 300, Dakhalia 8 zikiwemo dakhalia za wanaume za Chwaka Tumbe
na Paje Mtule pamoja na kuzifanyia ukarabati mkubwa na mdogo skuli 100 za
Msingi na Sekondari. Kujenga karakana (workshop) za Elimu ya Amali
Alisema katika Skuli 33 za Sekondari Unguja na Pemba (karakana 3 kwa
kila Wilaya) na kujenga uzio katika skuli ya Sekondari ya Hasnuu Makame na
Mohamed Juma Pindua.
Amesema kuimarisha matumizi ya tekonolojia katika kufundishia na kujifunzia kwa
kuziunganisha na mkonga wa taifa taaasi za Elimu zikiwemo; skuli 217 za
Sekondari, Vituo vya walimu 12 na Vituo vya Ubunifu wa Kisayansi (Hubs) 22
pamoja na kuzipatia vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa leo naomba niishie hapa kikubwa Mwenyenyezi Mungu akupe afya njema ili uendelee kuwahudumia wananchi wa Zanzibar huku ukijua kwamba hakuna kazi isiyo na changamoto kikubwa endelea kufanya kazi yako kwa kumtanguliza Mwenyezi Mungu ambaye hashindwi na chochote.. Kazi Iendelee.
Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa (katikati) akikata Utepe
kuashiria Ufunguzi wa Barabara ya Matemwe -Muyuni (7.6km) Wilaya ya
Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja. Wakati wa shamra shamra za
maadhimisho ya miaka 57 ya Mapinduzi Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, akiondoa
pazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Uzinduzi wa Mradi wa Barabara
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi .Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kufungua Mkutano wa
Jukwala la 13 la Biashara Zanzibar, lililofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya
Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar Oktoba 12,2024
Muonekano wa barabara ya Mchangani hadi Dogongwe (km 4.3)
visiwani Zanzibar, iliyojengwa kwa kiwango cha lami na kampuni ya IRIS
kwa kutumia teknolojia mbadala ya “chip seal” iliyotembelewa na wajumbe
wa Bodi ya Mfuko wa barabara (RFB), mwishoni mwa wiki kujifunza teknolojia
hiyo.

Sekta ya Mafuta na Gesi
Sekta ya Uvuvi na Mazao ya Baharini
No comments