ALEX MSAMA AMUOMBA RAIS SAMIA KUSAPOTI TAMASHA LA KUIOMBEA NCHI NA UCHAGUZI MKUU 2025
Wasanii wa Muziki wakishiriki hafla ya uzinduzi wa Tuzo ya Muziki wa Injili ya Afrika Mashariki iliyofanyika Ukumbi wa Cinema Mlimany City jijini Dar es Salaam Februari 27, 2025.
..............................................
Na Mwandishi
Wetu, Dar es Salaam
MDAU wa
Muziki wa Injili, Alex Msama amemuomba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kusapoti
tamasha la kuombea nchi, Amani, utulivu na uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba
2025 ili uwe wa mafanikio.
Msama alitoa
ombi hilo wakati wa uzinduzi wa Tuzo ya Muziki wa Injili za Afrika Mashariki
katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Cinema Mlimany City jijini Dar es Salaam
Februari 27, 2025 na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa muziki hapa nchini
wakiongozwa na mwanamuziki Mkongwe Mzee Cosmas Chidumule.
“Tunatarajia
kufanya tamasha kubwa nchi nzima la
kuiombea nchi Amani, utulivu na uchaguzi mkuu ambao utafanyika mwishoni mwa
mwaka huu hivyo tunakuomba Mama yetu utusaidie kutusapoti ili tamasha hilo
liweze kufanikiwa,” alisema Msama.
Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Sanaa, Wizara ya Habari Sanaa na Michezo, ambaye alikuwa mgeni
rasmi kwenye uzinduzi wa tuzo hiyo kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo Profesa Palamagamba Kabudi,
Dkt. Emmanuel Ishengoma alisema Serikali inatamani kuona kuwa licha ya muziki wa
injili kuburudisha na kumtukuza Mungu wangependa kuona unazaa ajira, inakuwa ni
uchumi na kuzalisha kipato na kuchangia katika pato la taifa.
“Sisi kama
Serikali tutahakikisha tunaendelea kuwajengea mazingira wezeshi ili muweze kunufaika kupitia fursa
mbalimbali,” alisema Ishengoma.
Alisema
Tanzania huenda ikawa ni moja ya nchi chache Afrika na duniani ambayo kila kitu
katika Sanaa kimeundiwa taasisi yake ya kukisimamia akitolea mfano ofisi ya haki miliki, bodi ya filamu, Chuo
cha TaSuba, mfuko wa kuwakopesha, mashirikisho mbalimbali na kadharika.
Kwa upande
wake Katibu Mkuu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Dkt. Kedmon Mapana lisema waimbaji wa nyimbo za injili ni wasanii kama walivyo wengine kutokana
na kuimba nyimbo zao kwa mpangilio unaoeleweka na kuwa Baraza la Sanaa Tanzania
linawahusu.
Aidha, Dkt.
Mapana aliwaomba wasanii hao kwenda kujisajili kwenye baraza hilo ili waweze
kutambulika, kuwa na kibali cha Basata na kuwa na haki na kueleza kuwa milango
yausajili ipo wazi.
Dkt. Mapana
alitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Muziki, Addo
November kwa kuvialika vyama mbalimbali vya muziki kushiriki kwenye uzinduzi
huo.
Muasisi wa tuzo
hizo Margaret Chacha akizungumza kwenye uzinduzi huo aliwataka wanamuziki
kupendana na kuwa kitu kimoja na kueleza kuwa baada ya kuzindua tuzo hizo
mpango wao ni kusongambele zaidi kutoka nchi nane zilizopo kwenye jumuiya hiyo
ya Afrika Mashariki na kusambaa nchi nyingine zaidi.
Naye Rais wa
Shirikisho la Muziki Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Muziki, Addo November, aliwataka wanamuzi kuwa na umoja na
upendo ambapo alitumia uzinduzi huo kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
kwa kazi kubwa aliyowafanyia kwa maboresho makubwa ikiwa ni pamoja kuweka kodi
kwenye kila vifaa vinavyohusu muziki vinapoingia nchini na fedha hizo
kuzielekeza kwa wasanii.
November alitumia nafasi hiyo kuwahimiza wasanii wote waliokopeshwa fedha hizo na Serikali kuzirejesha ili ziweze kukopeshwa kwa wengine.
Wannamuziki wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa, Wizara ya Habari Sanaa na Michezo, Dkt. Emmanuel Ishengoma ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo Profesa Palamagamba Kabudi,
Katibu Mkuu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Dkt. Kedmon Mapana akionesha umahiri wa kuserebuka kwenye hafla hiyo.
Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania na Mwenyekiti wa Cha cha Muziki, Addo November, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mdau wa wa Muziki wa Injili, Alex Msama akisalimiana na Muasisi wa tuzo hiyo, Margaret Chacha.
Katibu Mkuu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Dkt. Kedmon Mapana, akisalimiana na viongozi mbalimbali.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa, Wizara ya Habari Sanaa na Michezo, Dkt. Emmanuel Ishengoma, akisalimiana na viongozi mbalimbali na wadau wa muziki.
Picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.
Burudani ya nyimbo za injili ikitolewa.
Wanamuzi wa injili wakiserebuka.
Muimbaji wa nyimbo za Injili Jesca Magupa akiwajibika jukwaani.
Mserebuko ukiendelea jukwaani
Mwimbaji wa nyimbo za Injili Miriamu Mauki akitoa burudani.
Msanii wa muziki Fid Q akichangia jambo kwenye uzinduzi huo,
Wanamuziki wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Mwanamuziki Cosmas Chidumule na Addo November wakiimba kwenye uzinduzi huo.
Uzinduzi ukiendelea.
Uzinduzi wa tuzo hizo ukifanyika.
No comments