KATIBU TAWALA BUKOBA MJINI, KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WAINGIA MTAANI KUFANYA USAFI .
Katibu Tawala (DAS) Wilaya ya Bukoba Bi. Proscovia Mwambi akifanya usafi katika maeneo ya Bukoba mjini ikiwa ni utaratibu waliojiwekea wa kufanya usafi kila Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi kama Serikali ilivyoagiza.
...............................................
Na Mwandishi Wetu, Bukoba
KATIBU Tawala (DAS) Wilaya ya Bukoba Bi. Proscovia Mwambi akiambata
na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalaam wa wilaya hiyo kwa kushirikiana na viongozi wengine
wamefanya usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali wilayani humo
Shughuli hiyo ya kufanya usafi imefanyika Februari 22, 2025 kwa kushirikiana na
wananchi.
Akizungumza baada ya kufanya usafi usafi huo Mwambi alisema
wamefanya usafi huo kwa lengo la kuweka mazingira bora ndani ya wilaya hiyo
jambo ambalo litasaidia kuepuka uwezekanp wa kupata magonjwa ya mlipuko kama
vile ykuumwa matumbo na kipindupindu.
“ Zoezi hili la kufanya usafi ni endelevu na Serikali ya
Wilaya chini ya Mkuu wa Wilaya yetu ya Bukoba Mhe. Erasto Sima imekua ikikisisitiza
juu ya utunzaji wa mazingira hivyo ni wajibu kwa kila mmoja wetu kufanya usafi,”
alisema Mwambi.
Mwambi alisema kila Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi,
wanatakiwa kufanya usafi kama Serikali ilivyoagiza na kueleza kwamba Wilaya ya
Bukoba kwa mazingira safi inawezekana.
Katibu Tawala (DAS) Wilaya ya Bukoba Bi. Proscovia Mwambi na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufanya usafi.
Katibu Tawala (DAS) Wilaya ya Bukoba Bi. Proscovia Mwambi akiendelea kufanya usafi.
Usafi ukifanyika.
No comments