KILOSA WAANZA KUONJA ASALI YA HEWA UKAA, WAVUNA TANI 545, 433 SAWA NA SH.BILIONI 1.1
Shaka asema ni ukombozi mpya awahimiza wananchi kutumia fursa.
Wampa maua yake Rais Samia kwa ushajihishaji.
Mkuu wa Wilaya ya KIlosa, mkoani Morogoro, Shaka Hamdu Shaka, akizungumza katika kikao cha kamati ya uvunaji misitu kilichoketi Februari 7, 2025 wilayani humo.
...........................................
Na Mwandishi wetu Morogoro.
MKUU wa Wilaya ya KIlosa, Shaka Hamdu Shaka, amewataka
wakazi wa wilaya hiyo kujikita katika biashara ya hewa ukaa, huo ndio ukombozi
kwao kuanzia ngazi ya vijiji na halmashauri.
Akizungumza katika kikao cha kamati ya uvunaji misitu, Shaka
amesema kwa sasa utajiri mkubwa upo katika biashara hiyo na kusema mfano
umeonekana baada ya kazi kubwa iliyofanyika matokeo yake wameanza kuyaona.
Amesema waliingia katika majaribio na kuangaliwa kama
wanaweza kufanya biashara hiyo wakapiga hatua, anaamini watakwenda kuwa mfano
mzuri wa kusimamia rasilimali zilizopo katika wilaya hiyo.
“Ninaimani sana na ninyi kwamba mtakwenda kufanya mageuzi ya
kulinda na kutunza rasilimali tulizonazo ili tija iweze kuonekana, lazima
tukiri kwamba bado tunachangamoto, mfano mzuri ni migogoro kati ya kijiji na
kijiji, kamati za maliasili za kijiji fulani kuvamia kijiji fulani.
“Watu wamezigeuza rasilimali kuwa mali ya watu binafsi,
wanasimamia utunzaji misitu lakini wao wamekuwa ndio madalali wa kudalalia
rasimali hizo ziweze kuuzwa kiholela,” amesema.
Shaka amevipongeza vijiji 10 ambavyo vilifanya vizuri kwamba
wana faraja na kupata nguvu ya kuzungumza baada ya kuona namna jitihada
zilivyozaa matunda kuanzia mwaka 2023 hadi Februari mwaka huu.
"tunavujinia
mfaniko haya kwa sababu tulidhamiria na kuhakikisha tunatekeleza maelezo
ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan kututaka
kutumia vizuri fursa ya biashara ya hewa
ukaaa kwa kutunza mazingira na misitu yetu ili tija ionekane, tunamshkuru kwa
maono yake asali ya hewa ukaaa tumeanza kuionja Kilosa" alifafanua Shaka.
Ameeleza kuwa, kwa mara ya kwanza Wilaya hiyo imeweza
kuzalisha tani 545,433 ambazo ziitaingizia mapato ya sh. bilioni 1,171,478,458
ambapo ni gawio kulingana na mchanganuo wa mapato ambayo yamepatikana katika
misitu ya vijiji huku kijiji Cha Malolo, msiba na Mhenda vikifanya vizuri zaidi
katika kipindi cha 2023 mpaka Feb 2024.
“Tunauwezo wa kupunguza umaskini kupitia bishara hii ya hewa
ukaa, lakini pia tunauwezo wa kuifanya halmashauri hii kuwa ya mfano kupitia
mapato haya ya biashara ya hewa ukaaa kadri uwekezaji huu utakavyozidi
kutanuka” ameeleza.
Hata hivyo Shaka amepiga marufuku Uvunaji na usafishaji mashamba holela huku
akisitiza kuchukuliwa kwa hatua kali za kisheria kwa wote wataobainika kufanya
hivyo bila ya kuwa na vibali halali.
"Vijiji kwa kushirikiana na Halmashauri ya nendeni
mkaboreshe sheria ndogo ndogo za usimamizi wa misitu ili kuweka adhabu kali
zaidi kwa mtu yoyote atakayehusika na ukataji wa miti hovyo na uharibifu wa misitu"
alisema Shaka.Kikao hicho cha wadau wa misitu kikiendelea
Michango mbalimbali ikitolewa kwenye kikao hicho.
Wadau wa misitu na wataalam wa wilaya hiyo wakiwa kwenye kikao hicho.
Mkuu wa Wilaya ya KIlosa, mkoani Morogoro, Shaka Hamdu Shaka, akisisitiza jambo kwenye kikao hicho. Wengine kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Alto Mibike, Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Salome Mkinga na Kaimu Kamanda wa Uhifadhi wa wilaya hiyo.
No comments