WAZIRI WA AFYA AKAGUA GHALA LA DAWA MSD
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Vavere Tukai (kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja aliyoifanya Februari 6, 2025 jijini Dodoma.
.........................................
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama leo February 6, 2025
ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa ghala la Kisasa la
kuhifadhia bidhaa za afya linalojengwa na na Bohari ya Dawa (MSD) katika eneo
la Kizota, mkoani Dodoma.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhe. Mhagama amebainisha
kuwa serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imefanya mageuzi makubwa katika sekta
ya Afya, na imeendelea kujikita kwenye nguzo zinazo tuongoza za kimfuno
zinazopelekea Ubora wa huduma kwenye sekta ya Afya.
"Kazi zilizofanywa zinaonekana, na hata leo tumeona
uwekezaji mkubwa wa ghala la hili kubwa na la Kisasa ambalo lina Ubora wa
kimataifa, serikali imewekeza hapa zaidi ya Bilioni 23.7" kujenga ghala
hili lenye mita za Mraba 7,200. Alisema Mhagama.
Mhe. Mhagama ameongeza kuwa ujenzi huo pia umeendelea kwenye
Kanda ya Mtwara, ambapo zaidi ya Bilioni 18 zimetumika kukamilisha ujenzi, huku
akibainisha kwamba ujenzi huo pia utaendelea katika Kanda nyingine za MSD
ambazo ni Mwanza, Chato, Iringa, Moshi, Arusha na Songea.
"Lengo kubwa la jitihada hizi ni kuhakikisha bidhaa za
afya zinapatikana kwa wakati na kwa Ubora unaotakiwa, na zinahifadhiwa katika
mazingira yanayotakiwa, hivyo Bodi, menejimenti na Serikali ya Dkt. Samia
mmeupiga mwingi. alisisitiza Mhe. Mhagama.
Katika hatua nyingine Mhe. Mhagama ameupongeza uongozi wa
MSD kwa kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya nchini, ambapo amebainisha
kwamba hivi sasa upatikanaji huo umepanda hadi kufikia asilimia 83%.
Ameongeza kuwa MSD ni nyenzo muhimu katika uimarishaji wa
huduma za afya katika taifa letu.
Mhe. Mhagama ameeleza kuwa Wizara yake itaendelea
kushirikiana na MSD Ili kuhakikisha ndoto na maono haya ya kumkomboa mtanzania,
na kuweka usalama kwenye taifa letu yanatimia, kwani afya ya Mtanzania ni
usalama wa taifa letu.
Ziara ikiendelea.
Ziara ya ukaguzi wa ghala hilo ikiendelee.
Ukaguzi wa ghala hilo ukiendelea
No comments