WANAMUZIKI WANAWAKE WA MKOA WA ARUSHA KUNOGESHA SIKU YAO KWA BURUDANI YA AINA YAKE
...........................................
Na Dotto
Mwaibale, Arusha
WANAMUZIKI
Wanawake wa jiji la Arusha wamejipanga sawasawa kunogesha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake
Duniani kwa kuimba nyimbo bora ukiwepo wa maadhimisho hayo.
Mwanamuziki
Maarufu jijini Arusha, Patricia Kanya ambaye ameshiriki katika
wimbo huo maalum wa siku hiyo muhimu kwa wanawake akizungumza na waandishi wa
habari jijini Arusha Machi 1, 2025 alisema siku hiyo Arusha itasimama na kupata
burudani ya aina yake.
“ Wanawake
wanamuziki wa Mkoa wa Arusha tumejipanga vilivyo kutoa nyimbo
kadhaa tulizo ziandaa ukiwepo wimbo maalumu kwa ajili ya siku yetu hiyo,”
alisema Kanya.
Alisema
baadhi ya nyimbo hizo zina maudhui ya kuunga mkono jitihada kubwa zinazofanywa
na Rais wa Jamhuri ya Muunguno wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan za
kuwaletea wananchi maendeleo katika sekta mbalimbali na kuhamasisha wananchi
kuungamkono jitihada hizo.
“ Tayari tumekwisha
rekodi baadhi ya nyimbo ambazo zinahamasisha kudumisha Amani na Utulivu wa nchi
na kuendelea kudumisha ushirikiano hasa katika kipindi hiki ambacho nchi
inajiandaa kufanya uchaguzi mkuu mwezi Oktoba 2025,” alisema Kanya.
Alisema
Wanawake wote wa Mkoa wa Arusha chini ya Mkuu wao wa Mkoa, Paul Mkonda hawata
poa kumsemea Rais Samia Suluhu Hassan kwa mambo makubwa aliyoyafanya ya
maendeleo kwa ajili ya wananchi wa Tanzania na kueleza kwamba wimbo wao huo
maalumu utakuwa na kaulimbiu ya maadhimisho ya siku hiyo mahususi kwa ajili ya
wanawake duniani 2025.
Maadhimisho
ya Siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka huu yanatarajiwa kufanyika Uwanja wa
Sheikh Amri Abed jijini Arusha ambapo kilele chake ni Machi 8, 2025 na mgeni
rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu
Hassan.
No comments