Breaking News

MKUTANO WA KANDA WA TATHMINI YA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI NA MTOTO WAANZA NJOMBE

Mwenyekiti wa Mkutano  wa Kanda wa Tathmini ya Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto Kanda ya Nyanda za Juu Kusini    ambaye ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dr. Juma Mfanga, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Aprili 14, 2025.

......................................

Na. Chrispin Kalinga, Njombe 

MKUTANO wa Kanda wa Tathmini ya Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto kwa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini umefanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe, ukiwakutanisha wataalamu na wawakilishi kutoka mikoa ya Njombe, Iringa na Ruvuma.

Mkutano huu ambao utakuwa wa siku mbili, unalenga kufanya tathmini ya utekelezaji wa huduma za afya ya uzazi na mtoto katika kipindi kilichopita na kuweka mikakati ya pamoja ya kuboresha huduma hizo kwa mwaka ujao.

Akizungumza wakati wa ufunguzi, Mwenyekiti wa Mkutano ambaye ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dr. Juma Mfanga, alisema:

 “Kupitia mkutano huu, tunaweka msingi wa maamuzi yatakayosaidia kuimarisha huduma za afya ya uzazi na mtoto katika kanda yetu. Ni muhimu kila mmoja wetu awe mkweli na mzalendo katika kutoa tathmini halisi,” alisema Dkt. Mfanga.

Taarifa zilizowasilishwa katika mkutano huo ni pamoja na: Taarifa ya huduma za afya ya uzazi na mtoto kwa kanda nzima,Taarifa kutoka kwa kila mkoa,Utekelezaji wa Mfumo wa M-Mama na Namna ya ukusanyaji wa damu salama. Mkutano huu unafanyika kwa siku mbili pamoja na  kufanya  mjadala wa kina na kuweka maazimio ya pamoja ya utekelezaji kwa mwaka unaofuata


Mawasilisho mbalimbali yakitolewa.
Taswira ya mkutano huo.
Mkutano huo ukiendelea.
Washiriki wakiwa kwenye mkutano huo.
Muonekano wa mkutano huo wakati ukifunguliwa.

 

No comments