MWANASHERIA VICKY MBUNDE: KUANDIKA WOSIA SIYO UCHURO
Mwanasheria Baraka Chipamba kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT), Baraka Chipamba, akitoa elimu kuhusu umuhimu wa kufungua mirathi baada ya marehemu kufariki wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Magomeni Bagamoyo mkoani Pwani Aprili 25, 2025.
................................................
N Mwandishi Wetu, Bagamoyo
Mwanasheria Vicky Mbunde kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT), amesema kuandika wosia siyo uchuro bali unasaidia kuondoa migogoro ya kugombea mali zilizoachwa na marehemu.
Hayo yalibainishwa na mwanasheria
huyo Aprili 25, 2025 wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Magomeni mjini
Bagamoyo Mkoa wa Pwani wakati akitoa elimu inayohusu umuhimu wa kuandika Wosia pamoja
na kujiepusha na makosa mbalimbali ya kimtandao.
Alisema makosa ya kimtandao yamekuwa
yakifanyika kwa kutumia vifaa vya kielektroniki kama kompyuta, simu janja,
vishikwambi na Teknolojia ya Mawasiliano ya Habari (TEHAMA).
Mbunde alisema wosia ni nyaraka ya kisheria ambayo inaonyesha matakwa na maagizo ya mtu kuhusu namna mali yake itakavyogawiwa baada ya kifo chake na kuwa unaweza kujumuisha maelekezo kuhusu jinsi mali itakavyogawiwa kwa warithi, uteuzi wa wasimamizi wa mali, na mambo mengine yanayohusiana na urithi wa mtu husika.
“ Malengo ya kuandika wosia ni kuhakikisha kwamba matakwa ya mtu yatatekelezwa ipasavyo baada ya kifo chake na kuwa unaweza kuwa na athari za kisheria na unaweza kutambulika na mahakama mara tu baada ya kifo cha mtu aliyeandika wosia huo,” alisema Mbunde.
Mbunde alisema wosia unaweza kujumuisha mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na uteuzi wa warithi na kuonyesha ni nani atakayepokea mali za marehemu.
Alisema mtu anaweza kuteua watu wa kusimamia mali zake na kutekeleza matakwa yake kama watekelezaji wa wosia ambao unaweza kuainisha jinsi mali inavyopaswa kutumika, kugawanywa, au kuhamishwa kifedha.
Mwanasheria wa Tume hiyo, Baraka
Chipamba akizungumzia utaratibu wa kufungua mirathi alisema inategemeana kama
marehemu aliacha wosia au hakuacha wosia.
Alisema
kama marehemu aliacha wosia na kumchachagua mtu wa kusimamia na kugawa mirathi
yake baada ya yeye kufariki, ataomba mahakamani kuthibitisha wosia huo.
Aliongeza
kuwa kama hakuna wosia, hatua ya kwanza ni kuchagua msimamizi wa mirathi.
ambaye ndugu wa marehemu watalipendekeza jina lake ili asimamie mirathi.
Alisema kazi ya msimamizi wa mirathi ni kufungua Mahakamani shauri la maombi ya
kusimamia mirathi, kubainisha, kukusanya na kuhifadhi mali za marehemu, kulipa
madeni yaliyoachwa na marehemu na kugawa kilichobaki kwa warithi halali.
Chipamba
alisema siyo kila mahakama inaweza kusikiliza kesi hizo za mirathi ambapo
amezitaja mahakama ambazozinasikiliza mashauri hayo kuwa ni Mahakama ya Mwanzo,
Mahakama ya Wilaya. Mahakama ya Hakimu Mteule na Mahakama Kuu.
Alisema
unaweza kwenda Mahakama ya Mwanzo kama mirathi inahusisha sheria za
Kimila au za Kiislam na hiyo haijalishi thamani na ukubwa wa mirathi
husika hivyo kama wewe ni Mkristo, usiende Mahakama ya Mwanzo na utaenda
Mahakama ya Mwanzo iwapo sheria inayotumika kwenye hiyo mirathi ni ya Kimila au
Kiislam.
Aidha
Chipamba alisema Mahakama ya Wilaya inasikiliza mashauri ya mirathi ambayo haizidi Sh.100,000,000 kwa hiyo
chochote chenye thamani ya kuanzia sifuri mpaka million mia ni shauri dogo ambalo litasikilizwa.
“ Usiende Mahakama ya Mwanzo, hata kama mirathi ni fedha ndogo. Utatakiwa kwenda Mahakama ya iwapo tu sheria inayotumika ni ya kimila au kiislam,” alisema Chipamba.
Mwanasheria Vicky Mbunde kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT),Vick Mbunde akitoa elimu kuhusu umuhimu wa kuandika Wosia kabla ya kifo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Magomeni Bagamoyo mkoani Pwani Aprili 25, 2025.
Mwanasheria Vicky Mbunde kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT), Vick Mbunde, akigawa vipeperushi kwa wananchi wa Kata ya Magomeni wilayani Bagamoyo.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Magomeni, Mwajuma Yombe, akizungumza wakati wa mafunzo hayo.Mkazi wa Kata ya Magomeni, Tecra Philipo, akiuliza swali wakati wa utoaji wa elimu hiyo
Walimu wa Shule ya Sekondari ya Hassanali Damji wakishiriki kupata elimu ya sheria kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Dunda, Judith Mayunga, akitoa maelezo wakati wa utoaji wa elimu ya masuala ya mirathi wakati ilipokuwa ikitolewa kwa wafanyabiashara wa Soko la Samaki wilayani Bagamoyo.
Mwanasheria Baraka Chipamba kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT), akitoa elimu kuhusu umuhimu wa kufungua mirathi kwa wafanyabiashara wa Soko la Samaki Wilaya ya Bagamoyo.Mwanasheria kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT),Baraka Chipamba, akitoa elimu kuhusu umuhimu wa kufungua mirathi kwa walimu wa Shule ya Sekondari ya Hassanali Damji.
Wananchi wa Kata ya Magomeni wakipata elimu ya sheria kuhusu mirathi na kuandika wosia.
Elimu ikitolewa.
Mkazi wa Kata ya Magomeni, Seif Chama akiuliza swali.
Maswali yakiulizwa likiwemo matapeli wanawezaje kusajili laini za simu zaidi ya 100 wakati sheria hairuhusu?
Wananchi wa Kata ya magomeni wakiwa wameshika vipeperushi vya Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania wakati wa upokeaji wa elimu hiyo.
Viongozi wakiwa meza kuu wakati wa utoaji wa elimu hiyo Shule ya Sekondari ya Hassanali Damji.
Taswira ya utoaji elimu Shule ya Sekondari ya Hasanali Damji.
Mkazi wa Kaole Selemani Iddi akiuliza maswali wakati wa mafunzo hayo.
No comments