MBUNGE WA MUHAMBWE, DKT. FLORENCE SAMIZI ATIMIZA AHADI SHULE YA MSINGI BITURANA
Mbunge wa Muhambwe, Dkt. Florence Samizi.
.........................................
Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Ndg Dorice Faida Nsekela, amekabidhi Photocopy Machine aina Cannon IR 2224 yenye Gharama ya Tsh, 1750,000/= katika Shule ya Msingi Biturana, ambayo aliahidi Mhe. Dkt. Florence George Samizi. Ikilenga kusaidia kuondoa Gharama mbalimbali na usumbufu wa kutoa Copy Shuleni hapo.
Mkuu wa Shule hiyo Salvatory Muganga na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Biturana akiwemo Mhe. Barnabas Shedrack Baranzila {Diwani} wamemshukuru Mbunge kwa kutimiza ahadi aliyoahidi kisha wakimtakia mitano tena ya uwakilishi wa wananchi wa Muhambwe 2025-2030 na kuahidi ifikapo Oktoba Mwaka huu kumpa kura za kishindo.
No comments