BARRICK YADHAMINI MAADHIMISHO YA WIKI YA UTAFITI NA UVUMBUZI UDSM
.......................................
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KATIKA mwendelezo wa dhamira yake ya kuendeleza vipaji na kukuza utafiti nchini, kampuni ya
Barrick nchini imekuwa mmoja wa wadhamini wa maadhimisho ya kumi ya wiki ya
Utafiti na Uvumbuzi uliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo
imetunukiwa cheti cha tuzo kutokana na udhamini huo.
Katika maadhimisho ya mwaka huu Barrick imetoa shilingi
milioni 10 kwa mmoja wa washindi katika
utafiti Dkt. Juma Mmongoyo, kutoka
Mkwawa University College of education (MUCE) kwa mradi wake wa utafiti
kuhusu “Mbinu za kudhibiti mdudu mharibifu wa nyanya kwa ajili ya ukuaji wa zao
la nyanya mkoani Iringa.
Barrick mbali na udhamini huo imekuwa imekuwa ikidhamini
programu mbalimbali za utafiti ,uvumbuzi,na inazo programu za mafunzo ya vitendo kwa
wanafunzi wanaosoma katika vyuo vikuu na vya kati kwenye migodi yake nchini ya
North Mara na Bulyanhulu ambayo inaiendesha kwa ubia na Serikali kupitia
kampuni ya Twiga Minerals pia imekuwa kila mwaka ikifadhili semina za
kuwajengea wanafunzi wa vyuo vikuu uwezo kupitia taasisi ya AIESEC Tanzania.
Semina za Aiesec zinazoendelea katika vyuo vikuu mbalimbali
nchini zinazidi kuwapatia Wanafunzi utambuzi wa kujua fursa zilizopo nchini na
jinsi ya kuzitumia kuendeleza maisha yao,kupata ajira, kujiajiiri na
kutengeneza fursa za ajira.
Meneja wa Barrick nchini, Dkt Melkiory Ngido akiuliza swali
kutoka kwa vijana wa Chuo Kikuu kuhusu uvumbuzi na utafiti kwenye moja ya
mabanda kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwenye maadhimisho ya
kumi ya wiki ya utafiti na uvumbuzi ulimalizika jana , kushoto ni Mkurugenzi wa
Elimu ya Juu kutoka wizara ya Elimu , Sayansi na Teknolojia , Profesa peter
Msoffe
Post Comment
No comments