Breaking News

CCM YAITISHA MKUTANO MKUU MAALUMU, AJENDA KUU MAREKEBISHO MADOGO YA KATIBA

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla, akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 25, 2025 Jijini Dodoma.

...................................

Na Dotto Mwaibale

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kesho Julai 26, 2025 kinatarajia kufanya mkutano mkuu maalumu wa chama hicho Taifa. 

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, CP Amos Makalla amesema mkutano huo utafanyika kwa njia ya mtandao na kueleza kuwa maandalizi yake yamekamilika kuanzia katika wilaya na mikoa yote nchini.

Makalla amesema mkutano huo utafanyika kutokea Jijini Dodoma na utatanguliwa na vikao vya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa,, huku ajenda kuu ikiwa ni marekebisho madogo ya Katiba ya chama hicho. 

No comments