Breaking News

DC MSANDO: NGO'S MNAPASWA KUWA WAWAZI, KUJISAJILI, KUWAJIBIKA

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Albert Msando, akihutubia kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa kongamano la mwaka la mashirika yasiyo ya kiserikali liliofanyika katika ukumbi wa maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo Julai 25, 2025.

..................................................

Na Kelvin Kijo, Dar es Salaam

Mashirika yasiyo ya kiserikali nchini yametakiwa kutogeuza taasisi hizo kama miradi binafsi na badala yake wajikite katika kuwaletea wananchi maendeleo. 

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Wakili Albert Msando akiwa amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Challamilaa leo wakati wa kongamano la mwaka la mashirika yasiyo ya kiserikali liliofanyika katika ukumbi wa maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Msando amesema kumekuwa na kasumba kwa baadhi ya viongozi wa mashirika yasiyo ya kiserikali kutunga sheria na sera za miradi ambazo hazigusi maslahi ya taifa hivyo kushindwa kuwafikia wananchi wenye changamoto katika jamii.

“epukeni kutengeneza taarifa badala yake muifikie jamii kuyaibua matatizo yao na kuyatatua kwa kuweka rikodi sahihi kutoka kwa wananchi na changamoto wanazopitia ikiwamo changamoto ya lishe, mama wajawazito, uhaba wa taulo za kike, vijana na madawa ya kulevya, mikakati ya kutatua na mafanikio yaliyopatikana”

Awali mwakilishi wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NACONGO) Bi. Jovina ameyataja baadhi ya mafanikio kutoka kwenye mashirika mbalimbali katika kuifikia jamii.

“tumeweza kuwajengea uwezo maafisa wetu juu ya maswala ya malezi, kuwawezesha watoto wa kike wenye mazingira magumu kufikiwa na taulo za kike, nauli pamoja na vifaa vya shule, kuwezesha wakulima wadogo wadogo, na kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana na mbinu za kutoka kwenye uraibu wa madawa ya kulevya” alisema Bi Jovina.

Kwa upande wake mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali linalofanya utafiti nchini (AGRIF) ndugu Matiasi Kabaje ameishukuru serikali kwa kuwafikia ili kuhakikisha mashirika yanapata uwezeshwaji. “katika kongamano hili tumepata elimu na uelewa mpana sana kushiriki katika maendeleo ya taifa letu kwa kulipa kodi na kutumia wadau wa miradi kwa uwazi” alisema Kabadi.

Kongamnao hilo la siku moja lilijikita kufanya tathamini ya mchango wa Mashirika Yasiyo Ya Kiserikali katika maendeleo ya taifa kuanzia mwaka 2020/2021 mpaka mwaka 2024/2025 kuangazia mafanikio, changamoto, fursa na matarajio.


Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Albert Msando, akiwa na watoa mada kwenye kngamano hilo.
Taswira ya kongamano hilo.
Kongamano likiendelea.
Viongozi wa mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi wa kongamano hilo, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Albert Msando.
 

No comments