Breaking News

DKT. MWAMBA ATETA NA MKURUGENZI ESRF

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akiagana na  Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Prof. Fortunata Makene (kushoto), baada ya kikao kilichofanyika ofisini kwake, Treasury Square, Jijini Dodoma.
..............................

Na. Farida Ramadhani, WF, Dodoma.


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Prof. Fortunata Makene, kuhusu ushirikiano kati ya Serikali na Taasisi hiyo katika maendeleo ya nchi hususan katika masuala ya kiuchumi na kijamii. 

Amekutana naye ofisini kwake jijini Dodoma, ambapo alimwelezea maeneo ya kipaumbele nchini yanaongozwa kwa muda mrefu na Dira ya Maendeleo ya Taifa, kwa muda wa kati kupitia Mipango ya Maendeleo ya Miaka Mitano, na kwa muda mfupi kupitia Mpango wa Maendeleo wa kila Mwaka.

Miongoni mwa vipaumbele hivyo ni kuongeza nafasi za ajira, kupunguza kwa kiasi kikubwa viwango vya umaskini, na kuongeza mauzo ya nje na hivyo kuchangia kuchochea maendeleo jamii na nchi kwa ujumla.

No comments