UJENZI CHUO CHA MWALIMU NYERERE KAMPASI YA PEMBA UNAENDELEA
Muonekano wa ujenzi wa Chuo cha Mwalimu Nyerere Kampasi ya Pemba.
.......................................
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
SERIKALI inaendelea na Ujenzi wa miundombinu katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere - Kampasi ya Pemba ambapo ujenzi wa jengo la utawala umefikia asilimia 95 na ukumbi wa mikutano umefikia asilimia 50.
Aidha, imeendelea na ujenzi wa hosteli mbili (2) zenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 768 kila moja katika Kampasi ya Karume – Zanzibar ambapo ujenzi umefikia asilimia 52. Vilevile, imeendelea na ujenzi wa maktaba yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 2,500 na ukumbi wa mihadhara utakaohudumia wanafunzi 1,000 kwa wakati mmoja, katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni ambapo ujenzi umefikia asilimia 42.
No comments