WANANCHI 140 KAGERA WAPATIWA MAFUNZO YA UFUGAJI SAMAKI
.......................................................
Na Mwandishi Wetu, Kagera
Wananchi zaidi ya 140 mkoani Kagera wamehudhuria mafunzo ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba ili kuongeza uzalishaji wa samaki kutoka tani 32,349 zinazozalishwa sasa.
Akifungua mafunzo hayo Mheshimiwa Hajjat Fatma A. Mwassa Mkuu wa mkoa wa Kagera amewataka wananchi hao kuzingatia mafunzo ya ufugaji wa samaki ili kujikomboa na umasikini na kukuza uchumi wa mkoa wa Kagera na Taifa kwaujumla.
Mafunzo ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba yanafanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera kwa siku mbili Julai 10 hadi 11, 2025 na yanaendeshwa na wataalam kutoka Wizara ya mifugo na uvuvi .
Tayari Serikali mkoani Kagera imetenga maeneo 12 yanayofaa kwaajili ya vizimba vya samaki na tayari vimba 52 vimesimikwa. Aidha, Serikali ya Awamu ya Sita inatoa mikopo ya shilingi milioni 10 kwa kila kizimba kwaajili ya kulipia gharama za vibali na upimaji.
Ikimbukwe kuwa kizimba kimoja chenye ukubwa wa mita za mraba 256 kina uwezo wa kuzalisha tani 14 kwa muda wa miezi saba. Tayari mikopo ya shilingi bilioni 1.5 imetolewa na Serikali ya Awamu ya Sita kwaajili ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba na zana bora za uvuvi mkoani Kagera.
No comments