KANISA LA ABC LAANDIKA HISTORIA
Maandamano ya Kongamano Maalum la uwekaji wakfu wa maaskofu wanne, maaskofu waangalizi wa makanisa watatu na wachungaji 16 wa Kanisa la Abundant Blessings Church (ABC), yakiongozwa na wabeba bendera ya Taifa Teule la Israel, Bendera ya Taifa la Tanzania na Bendera ya Wanamaombi wa Afrika. Kongamano hilo lilifanyika Septemba 14, 2025.
................................................
Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam
KANISA la Abundant Blessings Church (ABC) lenye makao yake
makuu Jijini Dar es Salaam limeandika historia kubwa tangu kuanzishwa kwake
ambapo jana (Septemba 14, 2025) limepata maaskofu wanne, waangalizi wa kanisa
watatu na wachungaji 16 ambao wamewekwa wakfu.
Hafla ya kuwekewa wakfu maaskofu hao ilifanyika katika kongamano maalum la uwekaji wakfu lililofanyika Viwanja vya Chuo cha Biblia cha kanisa hilo kilichopo eneo la Kinyerezi kwa Makofia Ilala Jijini Dar es Salaam na kuongonzwa na Askofu Mkuu wa Huduma ya Kimataifa ya Harvest Intercontinental Church- Olney, USA, Darlingston Johnson.
Kongamano hilo lilihudhuriwa na mamia ya waumini wa kanisa hilo kutoka katika baadhi
ya mikoa sanjari na wageni waalikwa kutoka nje ya nchi wakiwemo maaskofu,
wachungaji na watu maarufu.
Askofu Johnson akizungumza na maaskofu hao na wachungaji aliwataka kwenda kuwa mfano bora wa kuhubiri neno la Mungu kwa ujasiri bila ya kuogopa huku wakitetea kwa nguvu imani ya dini ya kikristo.
“Nendeni mkautetee ukristo kama walivyofanya wenzetu ambao walikuwa tayari kuuawa kwa ajili ya kristo nanyi mkafanye hivyo,” alisema Askofu Johnson.
Askofu Mkuu wa kanisa hilo Mchungaji Flaston Ndabila alisema mwaka 2014 kanisa hilo lilianza kutoa huduma na mwaka 2019 ndipo lilipopata usajili kutoka Serikalini.
“Tunamshukuru sana Mungu wa mbingu nanchi kwa ajili ya ya mafanikio haya kwani ndani ya miaka 10 tangu lianze kanisa letu tumeweza kuwasimika maaskofu wanne, waangalizi wa kanisa watatu na wachungaji 16,” alisema Ndabila.
Alisema maaskofu waliowekwa wakfu ni wa kanda ya kusini, kanda ya ziwa, kanda ya mashariki na kanda ya kati.
Ndabila alisema tukio hilo lilikuwa la baraka sana kwani walikuwa na ugeni kutoka Marekani ambapo ametoka Askofu Darlingston Johnson ambaye aliongoza kongamano hilo.
Aliwataja wageni waliohudhuria tukio hilo ni Askofu Daniel Alain Njoya kutoka Cameroon, Askofu Mark Kairuki kutoka Kenya na wengine kutoka Burundi na Afrika Kusini akiwepo Mchungaji Dkt. Nicku Kyungu Mordi Rais wa Huduma ya I GO Africa for Jesus kutoka Marekani.
Maaskofu wengine walihudhuria konagamano hilo ni Askofu David Mwasota, Askofu James Mwaipyana, Askofu Amani Mwakyeja na Askofu Amon Lukama.
Maaskofu waliowekwa wakfu ni Cosmas Nchimbi, Prince Rubeya, John Muhembano na Nathaniel Ndabila ambapo Maaskofu waangalizi ni Lois Milyango, George Ntara na Joel Msalila.
Kwa upande wa wachungaji ni Alex Nyangoko, Oscar Mwampashi, Justin Kamesa, Boniphace Solomon, Dickson Malali, Emmanuel Shukrani, Gelvas Silondwa, Frank Ndabila, Paul Bundala, Steward Mkeng’enwa, James Mtunda, Denis Kinyaga, Onesmo Chunguke, Method Mloka, Edward Mhoja na Sabinus Mhagama.
Aidha, Askofu Ndabila alitumia nafasi hiyo kuishukuru Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ushirikiano mkubwa wanaoupata kupitia Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Mandela Tabata lilipo kanisa hilo.
Kongamano hilo lilinogeshwa na Mass kwaya ya kanisa hilo pamoja na kwaya ya watoto wa Sander School.
Askofu Mkuu wa Huduma ya Kimataifa ya Harvest Intercontinental Church- Olney, USA, Darlingston Johnson, akimvika vazi la kiaskofu, Askofu Nathaniel Ndabila baada ya kuwekewa wakfu katika kongamano hilo.Askofu Mkuu wa Huduma ya Kimataifa ya Harvest Intercontinental Church- Olney, USA, Darlingston Johnson, akiongoza maombi ya kuwaombea maaskofu waliopata wakfu akishirikiana na maaskofu wenzake wa Tanzania na kutoka nchi nyingine mbalimbali.
Askofu Mkuu wa Kanisa la ABC, Flaston Ndabila na mkewe wakiwa na Askofu Daniel Alain Njoya kutoka Cameroon.
Askofu Mark Kairuki kutoka nchini Kenya akizungumza kwenye kongamano hilo.
Askofu Mkuu wa Huduma ya Kimataifa ya Harvest Intercontinental Church- Olney, USA, Darlingston Johnson, akimjazi nguvu za imani Askofu Mkuu wa Kanisa la ABC, Flaston Ndabila. Katikati ni Mchungaji Dkt. Nicku Kyungu Mordi Rais wa Huduma ya I GO Africa for Jesus kutoka Marekani.
Askofu Mkuu wa Kanisa la ABC, Flaston Ndabila akimpongeza Askofu Mwangalizi wa kanisa hilo, Lois Milyango baada ya kuwekwa wakfu. Katikati ni Katibu Mkuu wa kanisa hilo, Peter Sifi ambaye alikuwa anaongoza itifaki katika kongamano hilo.
Wake za maaskofu hao wateule wakifuatilia kongamano hilo.
Waimbaji wa Mass Choir ya kanisa hilo wakiimba nyimbo za kusifu kwenye kongamano hilo.
Mwanasheria wa kanisa hilo, Jane Magigita akiwa katika ubora wake wakati wa kongamano hilo.
Shangazi wa Askofu Mkuu wa Kanisa la ABC, Sekela Ndabila (kulia), akiwa na mtoto wake Modester Mbwile kwenye kongamano hilo.
Wake wa maaskofu wateule wakiwa kwenye maandamano wakati wa kongamano hilo.
Matukio mbalimbali yakichukuliwa na wapiga picha binafsi.
Maandamano yakifanyika kabla ya kuanza kwa kongamano hilo.
Maandamano yakifanyika.
Maaskofu wateule wakiwa kwenye kongamano hilo. Kutoka kushoto ni Cosmas Nchimbi, Prince Rubeya, John Muhembano na Nathaniel Ndabila
Askofu Amani Lukama akiteta jambo na Mchungaji Dkt. Nicku Kyungu Mordi Rais wa Huduma ya I GO Africa for Jesus kutoka Marekani. .
Maaskofu wakiwa kwenye kongamano hilo.
Maaskofu wakiwa kwenye kongamano la kuwekwa wakfu. Kutoka kushoto ni Cosmas Nchimbi, Prince Rubeya, John Muhembano na Nathaniel Ndabila.
Kongamano hilo likiendelea.
Maaskofu wakiwaombea maaskofu wateule.
Wake wa maaskofu hao na wachungaji wakiwa kwenye maombi.
Maaskofu hao wateule wakiombewa.
Rais wa Huduma ya Kimataifa ya Harvest Intercontinental Church- Olney, USA, Askofu Darlingston Johnson. akiwasisitizia jambo maaskofu hao wateule.
Maaskofu wateule wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi.
Maombi zaidi yakifanyika.
Askofu Mkuu wa Huduma ya Kimataifa ya Harvest Intercontinental Church- Olney, USA, Darlingston Johnson. akiwaombea wachungaji waliowekewa wakfu wa kuwa waangalizi wa kanisa hilo.
Askofu Mkuu wa kanisa la ABC, Flaston Ndabila akiomba kwa hisia kali alipokuwa akiwaombea wachungaji waangalizi wa kanisa hilo.
Waangalizi wa kanisa wakiwekwa wakfu. Kutoka kushoto ni Joel Msalila, George Ntara na Lois Milyango.
Mwangalizi wa kanisa hilo Lois Milyango akipongezwa na mume wake baada ya kuwekwa wakfu wa kuwa mwangalizi wa kanisa hilo.
Askofu Mkuu wa Kanisa la ABC, Flaston Ndabila (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na maaskofu wateule na waangalizi wa kanisa hilo baada ya kuwekwa wakfu.
Wachungaji 16 wa kanisa hilo wakiwekwa wakfu.
Wachungaji wakipakwa mafuta na Askofu Mkuu wa Huduma ya Kimataifa ya Harvest Intercontinental Church- Olney, USA, Darlingston Johnson.
Askofu Daniel Alain Njoya kutoka Cameroon akiwaombea na kuwapaka mafuta wachungaji hao.
Wachungaji wakivikwa kora ya kichungaji.
Taswira ya kongamano hilo.
Mpiga kinanda wa kanisa hilo, Dkt. Gadi Ndabila akiwajibika ipasavyo wakati wa kongamano hilo.
Wachungaji wakiwa mbele baada ya kuwekwa wakfu.
Wachungaji hao wakiwa na wenza wao baada ya kuwekwa wakfu.
Katibu Mkuu wa Kanisa hilo, Peter Sifi (wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na maaskofu wateule na maaskofu waangalizi wa kanisa hilo.
Picha ya pamoja na Waangalizi wa kanisa hilo.
Picha ya pamoja na maaskofu wateule .
Wachungaji na maaskofu wateule wakiwa katika foleni ya kupongenzwa.
Askofu Mkuu wa Huduma ya Kimataifa ya Harvest Intercontinental Church- Olney, USA, Darlingston Johnson. akiwapongeza wachungaji hao.
Askofu Mkuu wa Kanisa la ABC, Flaston Ndabila akiwapongeza wachungaji hao.
Mchungaji Dkt. Nicku Kyungu Mordi Rais wa Huduma ya I GO Africa for Jesus kutoka Marekani akiwapongeza wachungaji hao.
Askofu Mark Kairuki kutoka Kenya akiwapongeza wachungaji hao.
Wachungaji wakipongezwa na ndugu, jamaa na marafiki zao.
No comments