Breaking News

MAKAMU WA RAIS AMPOKEA ALIYEKUWA MAKAMU MWENYEKITI KANDA YA KATI CHADEMA AKIHAMIA CCM

Aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Kati Bw. Jackson Jingu, akivaa shati la CCM baada ya kuhamia  Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kupokelewa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmshauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango wakati wa Kikao cha Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Singida Oktoba 26, 2025.

....................................

Na Mwandishi Wetu, Singida

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmshauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango, leo tarehe 26 Oktoba 2025, amempokea aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Kati Bw. Jackson Jingu, aliyehamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa Kikao cha Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Singida. 

Kikao hicho kimefanyika Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Singida na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, ambaye pia ni mratibu wa kampeni za CCM Kanda ya kati, Dkt. Bashiru Ally Kakurwa. 

Akizungumza mara baada ya kujiunga na CCM, Ndugu Jackson Jingu, amewaasa wananchi kutoshiriki katika uvunjifu wa amani wala maandamano kwa kuwa wanaotoa wito wa maandamano hawatoshiriki na wengine hawatokuwepo nchini. Amesema utoaji wa matamko yanayoashiria uvunjifu wa amani yanayotolewa na baadhi ya vyama vya siasa yanapaswa kukemewa ili kulinda amani ya nchi.

Aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Kati Bw. Jackson Jingu, akivaa shati la CCM.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmshauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimpokea Jackson Jingu.
Jackson Jingu akipokelewa na viongozi mbalimbali.
Jingu akipokelewa.

Makamu wa Rais Philipo Mpango akipokelewa kwa ngoma za asili.
Mapokezi yakifanyika.
Mapokezi ya Makamu wa Rais yakifanyika mkoani Singida.
 

No comments