MAWAKALA WA HUDUMA ZA FEDHA MKALAMA WAWEKA MKAKATI KUZUIA FEDHA ZA RUSHWA
..............................................
Na
Dotto Mwaibale, Mkalama
MAWAKALA
watoa huduma za fedha Wilaya ya Mkalama mkoani Singida wamehimizana kutoa
taarifa ya fedha ambazo watazitilia mashaka kuwa ni za rushwa ambazo
zitafikishwa kwao kuzituma katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu utakaofanyika
wiki ijayo.
Hayo yalibainishwa na Wema Ndomba ambaye ni Wakala wa Huduma za Fedha kutoka Kijiji cha Nkalakala wakati akichangia mada katika Semina iliyoandaliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Mkalama Mkoa wa Singida.
Semina hiyo ilikuwa mahususi kwa Maafisa usafirishaji (Bodaboda) na Mawakala wa Huduma za Kifedha jinsi ya kukabiliana na vitendo vya rushwa katika kipindi cha uchaguzi mkuu utakaofanyika wiki ijayo.
“Mafunzo tuliyopata katika semina hii yametupa mbinu za kugundua fedha ambazo zitafikishwa kwenye maeneo yetu ya kazi ili tuzitume kwa watu wengine hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi hivyo mara tutakapo zitilia mashaka bila ya kuchelewa tutoe taarifa TAKUKURU kwa kwenda ofisini kwao au kupiga namba yao ya bure 113,” alisema Ndomba.
Alisema watu wengine ambao wanapaswa kutolewa taarifa ni wale ambao watawatilia mashaka baada ya kufika kwao na fedha nyingi ambazo zitakuwa na harufu kutakatishwa.
Ndomba aliwataka watoa huduma hao kupokea kwanza fedha kutoka kwa wateja wao ndipo wazitume ili kuepuka kutapeliwa kwani baadhi yao wamekuwa wakitapeliwa mara kwa mara.
Mawaka wa Huduma za Fedha na Maafisa Usafirishaji (Bodaboda), wakiwa kwenye semina hiyo.






.jpg)




No comments