DKT. TULIA ACKSON ARUDIA NJIANI MBIO ZA USPIKA WA BUNGE LA TANZANIA
Aliyekuwa Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson ametangaza kujiondoa rasmi katika kugombea nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) leo Novemba 07, 2025. Hii inamwachia nafasi Mussa Azzan Zungu na Stephen Julius Masele kuendelea na kinyang'anyiro hicho ndani ya CCM.
Katika kinyang'anyiro hicho wana CCM kadhaa wakiwemo vigogo wa chama hicho walijitokeza kuwania nafasi hiyo akiwemo Dkt Tulia Ackson, Mussa Zungu, Stephen Masele.
Vigogo wengine waliojitokeza ni pamoja na Mbunge wa Babati Vijijini Daniel Sillo, Profesa Paramagamba Kabudi na Mbunge wa Isimani William Lukuvi.






.jpg)




No comments