Breaking News

IDARA YA ITIKADI, UENEZI CCM YAKUTANA KUJADILI USIMAMIZI ILANI YA UCHAGUZI 2025/ 2030

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Samia Suluhu HassanMakamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa Dkt. Emmanuel Nchimbi ambaye sasa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakionesha ilani baada ya kuizindua Mei 30, 2025 Jijini Dodoma.
.......................................

Na Dotto Mwaibale, Dodoma

IDARA ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa chini ya Katibu wake Kenani Kihongosi imekutana Jijini Dodoma katika kikao kazi kwa lengo la kuanza usimamizi wa Ilani ya 2025/2030.

Kikao kazi hicho maalumu kilichofanyika Novemba 10, 2025 jijini Dodoma kimewahusisha wakuu wa Vitengo wa Idara ya Itikadi Uenezi na Mafunzo wa chama hicho pamoja na watumishi.

Kufanyika kwa kikao hicho ni hatua nzuri ya kuanza utekelezaji wake baada kumalizika kwa uchaguzi mkuu ambapo chama hicho kimepata ushindi wa kishindo.

Katika ilani hiyo kuna mambo kadhaa yatakayotekelezwa kwenye sekta ya elimu,barabara, afya, kilimo na uchumi.

Mwenyekiti wa CCM  Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan ndiye alizindua ilani hiyo ambayo itatekelezwa kwa miaka mitano.

Baada ya Uzinduzi huo Dkt Samia alimkabidhi nakala Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira, pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM kwa Upande wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa Dkt. Emmanuel Nchimbi ambaye sasa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa Kenani Kihongosi, akiongoza kikao hicho.
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa Kenani Kihongosi, akisisitiza jambo kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
 

No comments