WABUNGE WAJENGEWA UWEZO WA MASUALA MBALIMBALI
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Daniel Sillo akiongoza Mafunzo kwa Waheshimiwa Wabunge leo Novemba 17, 2025 Jijini Dodoma.
...................................
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameanza kupata mafunzo ya siku tano yenye lengo la kuwajengea uwezo kuhusu masuala mbalimbali.
Pamoja na mambo mengine mafunzo hayo yatawasaidia kujua uendeshaji wa bunge, umuhimu wa kamati za bunge na maadili ya viongozi.
Aidha, masuala mengine ambayo watajifunza kupitia mafunzo hayo ni Haki na Wajibu wa Wabunge, Diplomasia na Itifaki za Kibunge pamoja na Mahusiano ya kazi baina ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Bunge.
Mafunzo hayo yalifunguliwa na Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu na kuongozwa na Naibu Spika wa Bunge Mhe. Daniel Sillo.
Wabunge wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Mafunzo hayo yakiendelea.





.jpg)




No comments