WABUNGE WATEULE BUNGE LA 13 WATUA DODOMA WAANZA KUJISAJILI
Mbunge wa Jimbo la Ilongero mkoani Singida, Haiderali Gulamali akijisajili tayari kwa kushiriki Bunge la 13, litakaloanza rasmi Novemba 11, 2025.
|
Na Dotto Mwaibale, Dodoma WABUNGE wateule wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania wamekwisha wasili Dodoma na kuanzia leo Novemba 8 hadi 10, 2025 wameanza
kujisajili na kufanya taratibu nyingine za kiutawala, kabla ya kuanza rasmi kwa
vikao vya Bunge jipya Jumanne ya Novemba 11, 2025. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Bunge, Baraka
Leonard hivi karibuni ilieleza kuwa usajili wa wabunge hao wateule utafanyika
katika Ofisi za Bunge, ambapo watafanyiwa zoezi la upigaji picha na uhakiki wa
nyaraka mbalimbali. Moja ya jambo la kwanza litakalofanyika katika kikao cha kwanza cha mkutano wa kwanza wa Bunge la 13 kitahusisha kusomwa kwa tangazo la Rais la kuitisha Bunge, uchaguzi wa Spika, kiapo cha uaminifu kwa wabunge wote, kuthibitisha uteuzi wa Waziri Mkuu, uchaguzi wa Naibu Spika pamoja na ufunguzi rasmi wa Bunge jipya utakaofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wabunge hao wateule wametakiwa kufika wakiwa katika mavazi rasmi na kuwasilisha
nyaraka muhimu ikiwemo kitambulisho cha taifa na nakala yake, hati ya
kuchaguliwa pamoja na kadi ya benki yenye namba ya akaunti. |
Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini mkoani Manyara, Mhe. Emanuel John Kambay akijisajili.





.jpg)




No comments