WANU AMEIR ALA KIAPO BUNGENI JIJINI DODOMA
Mbunge wa Jimbo la Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja, Mhe. Wanu Hafidh Ameir akila kiapo Jijini Dodoma.
..................................
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Mbunge wa Jimbo la Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja, Mhe. Wanu Hafidh Ameir leo Novemba 11 Novemba, 2025 amekula kiapo cha kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kipindi cha miaka mitano (2025-2030) katika Bunge la 13.
Mhe. Wanu Hafidh Ameir ameungana na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kula kiapo mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu
Wanu Hafidh Ameir aliibuka na ushindi wa kishindo kwa kupata kura zaidi ya 18,000 zilizopigwa na wananchi wa Jimbo la Makunduchi huku akiwaacha mbali wapinzani wake walioambulia kura chache katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025.






.jpg)




No comments