Breaking News

AFISA TARAFA KATERERO BWANKU BWANKU ASHAURI MELI MPYA YA MV MWANZA KUPITA BANDARI YA KEMONDO

Itasaidia kupunguza nauli na kuwanufaisha wananchi

 Afisa Tarafa ya Katerero iliyopo Mkoa wa Kagera Bwanku Bwanku akichangia jambo  kwenye kikao baina ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO) na wadau wa Bandari za Kagera kilichofanyika jana mkoani humo.

.........................................

Na Mwandishi Wetu, Kagera. 

Afisa Tarafa ya Katerero iliyopo Mkoa wa Kagera Bwanku Bwanku ametoa ushauri mara Meli mpya ya MV Mwanza itakapoanza safari zake katika ukanda wa ziwa iwe na safari Bandari ya Kemondo jambo litakalosaidia kupunguza nauli kwa wananchi.

Bwanku Bwanku alitoa ombi hilo kwenye kikao baina ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO) na wadau wa Bandari za Kagera kikao hicho .

"Serikali ya Tanzania imekamilisha ujenzi wa Meli kubwa ya kisasa ya MV Mwanza iliyogharimu Bilioni 120 ikiwa na uwezo wa kubeba Tani 400 za mizigo na abiria 1,200 kwa wakati mmoja," alisema Bwanku Bwanku.

Bwanku alisema  Meli hiyo inatarajia kuanza safari zake rasmi katika Ziwa Victoria kuanzia Mwanza, Kagera na ukanda mzima wa Ziwa hivi karibuni.

 Disemba 19, 2025 ameshiriki kikao cha pamoja kati ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO) na wadau wa Bandari za Kagera, kikao hicho  kilihusu kupokea na kutoa maoni ya wadau kuhusu nauli za meli hiyo ambacho kilifanyika Hoteli ya ELCT- Bukoba Mjini.

Kikao hicho kilifunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Kanali (Mst) Hamis Maiga.

"Meli hiyo kubwa ikianza safari zake rasmi ni muhimu iwe na route ya Bandari ya Kemondo kinyume na ilivyo sasa ambapo TASAC na TASHICO wanapendekeza meli hiyo ifanye safari zake kutoka Mwanza hadi Bukoba na isipite Kemondo huku akishauri kupunguzwa ili wananchi wengi wafaidike na uwekezaji huo wa Serikali ya Tanzania," alisema Bwanku Bwanku..

Kikao kikiendelea
Bwanku Bwanku akisisitiza jambo kwenye kikao hicho
Kikao kikiendelea. 

No comments