SHANGWE LA SIKUKUU NA TANAPA SEASON 2 SAADANI KUNOGILE
Na Mashaka Kibaya,Aliyekuwa Hifadhi ya Taifa ya Saadani - Tanga.
........................................
SHANGWE la Sikukuu na TANAPA 2025, limeendelea kutikisa Hifadhi ya Taifa ya Saadani kwa wageni kutoka ndani na nje ya nchi kujitokeza kwa wingi kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii.
Kupitia tamasha hilo maalum kwa ajili ya kuhamasisha watu kufanya utalii, wageni wameendelea kujitokeza kutembelea hifadhi hiyo wakifurahia kuona wanyama wakiwemo Simba,Chui,Nyati,Tembo pia wanapata fursa ya kufurahia mandhari nzuri yenye uoto asilia.
Afisa Mwandamizi Kitengo cha utalii Hifadhi ya Taifa ya Saadani, Daud Gordon amesema, katika kipindi hiki cha Sikukuu, kupitia Shangwe la Sikukuu na Tanapa, wageni wanafurahia kufanya Utalii wa boti kwenye mto wami eneo ambalo nyika na bahari vinakutana.
"Tunashukuru Shangwe la Sikukuu na Tanapa wageni wanaendelea kumiminika, wakifurahia Christmas kwa kutembelea vituvio vya utalii, kwenye mto wami waanafurahia kuona wanyama kama Viboko, Mamba na ndege wa aina tofauti waliopo" alisema Gordon.
Ameongeza kusema kuwa, katika hifadhi hiyo ya kipekee ambayo nyika na bahari zinapakana, matukio mbalimbali yataendelea kupamba 'Shangwe hilo la Sikukuu na Tanapa', ambapo wageni watapata fursa ya kutembelea fungu la mchanga 'Mafue' eneo ambalo wanandoa wanaweza kulitumia kufanya fungate.
Ametoa wito kwa watu kutembelea hifadhi hiyo ili kujionea maajabu yaliyopo, hatua ambayo pia ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, aliyeanza kuhamasisha watu kufanya Utalii kupitia filamu ya Royal Tour.
| Afisa Mwandamizi Kitengo cha Utalii Hifadhi ya Taifa ya Saadani Daud Gordon akizungumzia Shangwe la Sikukuu na Tanapa Season 2 lilivyotikisa kwa Mwaka huu 2025. |
Taswira ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani






.jpg)




No comments