WMA YATOA ELIMU YA VIPIMO KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI YA DKT. SAMIA DODOMA
Wanafunzi wa Dkt. Samia Dodoma Sekondari School wakipata mafunzo ya vipimo kutoka kwa wataalamu wa Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA), Februari 21, 2026 Jijini Dodoma.
.............................
Na Mwandishi Wetu - DODOMA
Wakala
wa Vipimo Tanzania (WMA) imetoa mafunzo ya vipimo kwa wanafunzi wa Dr.
Samia Dodoma Secondary School, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuongeza
uelewa kuhusu umuhimu wa vipimo sahihi katika biashara na maisha ya kila
siku.
Katika zoezi hilo, wanafunzi walipata fursa ya kujifunza
kuhusu dhima na majukumu ya Wakala huo, pamoja na namna unavyolinda
maslahi ya watumiaji na wafanyabiashara kwa kuhakikisha vipimo vinakuwa
sahihi na vya kuaminika.
Akizungumza baada ya
mafunzo hayo, Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa WMA, Veronica Simba,
amesema elimu ya vipimo itatolewa katika mikoa yote ya Tanzania Bara ili
kuhakikisha wanafunzi wengi zaidi wanapata uelewa wa matumizi sahihi ya
vipimo.
Amesema mpango huo unalenga kukuza uelewa wa masuala ya
vipimo kwa vijana, sambamba na kuimarisha utamaduni wa uadilifu na
uwajibikaji katika sekta ya biashara nchini.
Kwa upande wake,
Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Dodoma, Said Ibrahim, amesema mafunzo
hayo yanaenda sambamba na uanzishwaji wa Klabu za Vipimo mashuleni ili
kuendelea kuandaa mabalozi mahiri watakaotoa elimu ya vipimo shuleni na
katika jamii kwa ujumla.
“Kwa Dodoma tayari tumeshatoa mafunzo
katika shule mbili ambazo ni Shule ya Msingi Mtemi Mazengo na leo
tumetoa hapa katika Shule ya Sekondari ya Dkt. Samia Dodoma. Tunaamini
mabadiliko katika matumizi ya vipimo sahihi yataongezeka,” amesema Said.
Naye , Mwalimu Mussa
Madandi, ambaye pia ni mlezi wa Klabu ya Vipimo shuleni hapo, amesema
elimu hiyo wamekuwa wakiifundisha darasani, lakini mafunzo yaliyotolewa
na WMA yamewapa wanafunzi nafasi ya kujifunza kwa vitendo, jambo
litakalosaidia kuongeza uelewa na kuimarisha matumizi ya vipimo sahihi.
“Vipimo
ni somo tunalolifundisha karibu kila darasa, lakini leo wanafunzi
wamepata mafunzo kwa vitendo kutoka kwa wataalamu wenyewe. Naamini hali
hii itaongeza hamasa ya kuzingatia usahihi katika matumizi ya vipimo na
kuwafanya wawe mabalozi wazuri kwa wazazi wao na jamii inayowazunguka,”
amesema Mwalimu Madandi.
Mwanafunzi Itabangola Elias amesema
elimu hiyo imewasaidia kuelewa namna ya kutambua vipimo sahihi na
kujikinga dhidi ya udanganyifu unaoweza kujitokeza katika biashara.
Baada
ya mafunzo hayo, wanafunzi walishiriki kujibu maswali mbalimbali
kuhusiana na vipimo na shughuli za Wakala huo, ambapo waliofanya vizuri
walipatiwa zawadi mbalimbali kama sehemu ya kuwahamasisha kuendelea
kujifunza na kuwa mabalozi wa matumizi sahihi ya vipimo katika jamii.
Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa WMA, Veronica Simba, akizungumzia kuhusu elimu ya vipimo kutolewa katika mikoa yote ya Tanzania BaraMeneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Dodoma, Said Ibrahim, akizungumza.Mwalimu Mussa Madandi, ambaye pia ni mlezi wa Klabu ya Vipimo shuleni hapo, akizungumza.Mafisa wa WMA wakizungumza na wanafunzi hao (hawapo pichani)Wanafunzi wakikabidhiwa mabegi baada ya mafunzo.Mabegi yakikabidhiwa kwa wanafunzi.Mafunzo yakiendelea kutolewa.Picha ya pamoja na wanafunzi waliozawadiwa mabegi.














.jpg)




No comments