RAIS SAMIA ATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA DAR, KUSHEREHEKEA PASAKA
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo (kushoto), akikabidhi msaada uliotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa viongozi na wawakilishi wa Makao za kulelea Watoto Yatima na Wahitaji wa Wilaya ya Ilala akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya watoto hao kusherehekea Sikukuu ya Pasaka.
............................
Na Dotto Mwaibale
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa msaada wa mahitaji mbalimbali kwa watoto zaidi ya 500 wanaolelewa katika makao za watoto yatima na wenye uhitaji wa Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Sikukuu ya Pasaka.
Msaada huo ulikabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kwa viongozi wanaowakilisha makazo hizo za kulelea watoto hao.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mpogolo alimshukuru Rais Samia kwa moyo wake wa ukarimu na kujali makundi maalumu.
“Nachukua nafasi hii kwa niaba ya wananchi wa Ilala pamoja na viongozi wa makao ya kulelea watoto wenye uhitaji ndani ya Jiji la Dar es Salaam, hususan Wilaya ya Ilala, kutoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa moyo wake wa ukarimu na upendo kwa kutoa msaada huu,” alisema Mpogolo.
Aliongeza kuwa msaada huo umetolewa kufuatia kumalizika kwa mfungo wa Mwezi wa Ramadhani na Kwaresima, ambapo Rais ameonesha huruma na mshikamano kwa watoto hao katika kipindi hiki cha maadhimisho ya Pasaka.
“Sisi wana Ilala tunalithamini tendo hili la Mheshimiwa Rais, si kwa kile tulichokipata pekee, bali kwa dhamira yake ya kujumuika nasi katika maadhimisho ya Sikukuu ya Pasaka na kusherehekea pamoja na watoto zaidi ya 500 waliopo katika wilaya yetu ya Ilala.. Tutaendelea kumuombea dua kwa kazi kubwa anayoifanya kwa taifa,” alisema Mpogolo.
Kwa upande wake, Katibu wa Shirika la kulea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu la TANKIDS COMING HOME, Charles Wambura, alimshukuru Rais Samia kwa msaada huo uliowafikia katika kipindi cha Pasaka, akisema umeleta faraja kwa watoto hao.
Aidha, aliwashukuru viongozi wa ngazi mbalimbali kuanzia kata, wilaya hadi mkoa kwa kuendelea kutoa msaada na ushirikiano kwa makao hayo.
Naye Katibu wa Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Mwana kilichopo Vingunguti, Mtaa wa Mtakuja, Amidi Mangoma, alimpongeza Rais Samia kwa maono yake ya kuwasaidia watoto wenye uhitaji na kumuombea kwa Mungu ampe afya njema na maisha marefu ili aendelee kulitumikia taifa. 🙏✨
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, akikabidhi msaada huo kwa Katibu wa Kituo cha kulelea Watoto Yatima cha Mwana kilichopo Vingunguti Mtaa wa Mtakuja, Amidi Mangoma.
Charles Wambura ambaye ni Katibu wa Shirika la kulea watoto Yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kupitia kituo chao kiitwacho TANKIDS COMING HOME kilichopo Gongo la mboto alimshuru Rais Samia kwa msaada huo wakati huu wa Pasaka.
Bidhaa na vyaakula vilivyotolewa kwa ajili ya kundi hilo maalumu
Katibu wa Kituo cha kulelea Watoto Yatima cha Mwana kilichopo Vingunguti Mtaa wa Mtakuja, Amidi Mangoma, alimshukuru Rais Samia kwa msaada huo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, akikabidhi msaada huo kwa Katibu wa Kituo cha kulelea Watoto Yatima cha Mwana kilichopo Vingunguti Mtaa wa Mtakuja, Amidi Mangoma.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo akikabidhi msaada huo.
Ndoo zenye mafuta ya kula na viroba vya unga na mchele vikiwa tayari kukabidhiwa.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, akimkabidhi msaada huo kwa Charles Wambura ambaye ni Katibu wa Shirika la kulea watoto Yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kupitia kituo chao kiitwacho TANKIDS COMING HOME kilichopo Gongo la mboto.
Mbuzi huyo aliyetolewa kitoweo kwa ajili ya kundi hilo.
Mdaada huo ukipokelewa.
Msaada ukiwa tayari kupokelewa.
Taarifa hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale, simu namba 0754362990.












.jpg)




No comments