Breaking News

SHEREHE ZA KUHITIMU KAMBI YA JANDO KIJIJINI MSOGA KWA RAIS MSTAAFU DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE

Mchana wa tarehe 31 Desemba 2023 kijijini Msoga wilaya ya Chalinze mkoani Pwani ukoo wa Kikwete walikuwa na sherehe kubwa  ya jando na unyago.

 

Sherehe hiyo ilihusisha  wavulana 11 na wasichana 7, wakiwemo watoto wa  Mhe Ridhiwani Kikwete, Mbunge wa Chalinze na Naibu Waziri katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, na ndugu zake.

 

Wavulana na Wasichana hao waliotoka siku hiyo ni wajukuu wa Rais Mstaafu  Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na  kaka zake na dada zake.

 

Sherehe hizo zilizofana sana kwa nyimbo na ngoma za kitamaduni zilifanyika baada ya vijana hao kumaliza takriban wiki mbili za mafunzo maalum kwenye kambi yao porini kwa mujibu wa mila na desturi za kabila la Wakwere.

 

Kwa mujibu wa wanakijijij wa Msoga waliohudhuria sherehe hizo, Wakwere bado wanaendeza mila ya jando na unyago kwa wavulana na wasichana wao ili kulinda na kudumisha kwa vitendo mila na desturi zinazohakikisha mtoto au kijana wao, kabla ya kuingia katika umri wa ki-utu uzima, anapata maarifa au stadi za maisha zinazomfanya awe kijana shupavu, anayejitambua na anayewajibika kikamilifu katika jamii na taifa.





Vijana wakiwa porini wakipata mafunzo mbalimbali ya stadi za maisha kutoka kwa mangariba
Vijana wakitoka porini baada ya kuhitimu kambi ya mafunzo ya jando kijijini Msoga





Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na kuratibiwa na Mhe Ridhiwani Kikwete, Mbunge wa Chalinze ambaye pia ni Naibu Waziri katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakitembelea vijana kambini kwao usiku.
Mke wa Rais Mstaafu na Mbunge wa Mchinga Mhe. Mama Salma Kikwete akiongoza kinamama kucheza ngoma
Wasanii Mzee Jusuph wa Jahazi na Khalid Chikoraa wa Twanga Pwepeta walikuwepo
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akicheza ngoma

Vijana wakiwa kambini siku moja kabla ya kutoka wakisubiri kinyozi kuwanyoa nywele
Vijana wakiwa tayari kuelekea kwenye sherehe za kuhitimu mafunzo ya Jando


 Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa katika msherehe
Wakati wa kuingia kwenye sherehe vijana wanapita juu ya Ngariba wao aliyelala kwenye kitanda cha kamba

 

No comments