KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA MRADI WA SGR
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Na Dotto Mwaibale, (Singidani Blog)
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imeridhishwa
na kulipongeza Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa utelelezaji mzuri wa mradi wa
reli ya kisasa ya Standard Gauge (SGR )
Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Augustine Vuma akizungumza na waandishi wa
habari Machi 27, 2024 baada ya kamati hiyo kukagua na kuangalia majaribio ya mradi
huo kuanzia Dar es Salam hadi Morogoro alisema wameridhishwa na utekelezaji wake.
“ Tumeona jinsi Serikali ilivyofanya uwekezaji mkubwa na thamani halisu ya fedha
hakika TRC wana kila sababu ya kupongezwa,” alisema Vuma.
Vuma alisema kama kamati wameridhishwa na mradi huo kwani umetekelezwa
katika viwango vizuri na pia unavutia.
Akizungumzia kuhusu manufaa ya mradi huo alisema katika utekelezaji wake
umetoa ajira za moja kwa moja 30,000 na ajira za muda mfupi 150 ambazo zimewezesha
kipande cha zaidi ya Bilioni 350.
Aidha, Vuma alisema safari za treni hilo zitakapoanza zitaenda kupunguza
zaidi ya nusu wa muda wa magari inanayo hutumia kutoka Dar es Salaam kwenda
Morogoroza na kuwa gharama za usafirishaji wa mizigo zitapungua kwa asilimia
40.
Alisema viashiria vya kwisha kwa kazi hiyo vinavyoonekana vinakwenda
sanjari na maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kutaka mradi huo uanze
kufanya kazi Mwezi Julai mwaka huu kuwa ni sahihi kabisa.
“ kwaniaba ya Kamati kwanza
nimpongeze Rais wetu,D kt.Samiah suluhu Hassan, kwa kazi kubwa
iliyofanyika kwanza kwa kutoa fedha nyingi ambapo takribani Sh. Trioni 23
zitatumika kuutekeleza kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma ambapo tayari Serikali
imekwisha toa zaidi ya asilimia ya 40 ya fedha ndio maana unakwenda vizuri.
Vuma alitumia nafasi hiyo kuwapongeza wataalamu na wafanyakazi wote
waliofanikisha kazi hiyo ambapo alitoa rai kwa TRC kuitunza miundombinu ya
mradi huo na kuwasumamia wakandarasi kumalizia kazi ya kipande kilichobakia.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TRC, Ally Karavina
alisema watatekeleza agizo la Rais Samia la kuhakikisha kabla ya Julai mwaka
huu treni hilo linaanza kufanya kazi.
Mkurugenzi wa TRC, Masanja Kadogosa aliishukuru kamati hiyo ya bunge na
kueleza inahusiana na Serikali katika mashirika mbalimbali na hatua
iliyoichukua ya kwenda kuangalia tija ya fedha zilizotolea kutekeleza mradi
huo.
Alisema TRC ni taasisi ambayo imepewa fedha nyingi hivyo ujio wa kamati hiyo kwenda kukagua mradi huo ni wa muhimu sana na hasa baada ya kuridhika na utekeleezaji wake na kuwa wataendelea kuchapa kazi na kuhakikisha mwezi Julai unaanza kutoa huduma.Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TRC, Ally Karavina (kushoto) akifurahia jambo na Mkurugenzi wa TRC, Masanja Kadogosa wakati wa ziara ya kamati hiyo ya bunge wakiwa ndani ya treni ya SGR.Wabunge wakiwa ndani ya treni ya SGR kuelekea Morogoro wakati wa ziara hiyo. Kushoto ni Mbne wa Mpwapwa, George Mabina na Mbunge wa Manyoni Mashariki Dkt.Pius Chaya.
No comments