RAIS SAMIA ATEKELEZA UJENZI WA MIRADI KWA ASILIMIA 70
---------------------
Na Dotto Mwaibale, ( singidani blog )
PAMOJA na Sintofahamu ya Watanzania walio wengi juu ya miradi mbalimbali ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) ukiwemo wa Standard Gauge (SGR ) hatimaye Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameonesha kwa vitendo zaidi utekelezaji wa miradi hii takribani asilimia 70 hadi sasa.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo Masanja Kadogosa alisema kutokana na kazi hiyo kubwa
iliyofanywa na Rais Samia ameibuka kinara kwa ujenzi wa miundombinu ya Reli
nchini.
Kadogosa aliyasema hayo Machi 25, 2024 wakati
akizungumza na wahariri na waandishi wa
habari wa vyombo mbalimbali wakati akitoa taarifa ya utekelezaji
majukumu ya shirika hilo na mafanikio katika kipindi cha miaka mitatu ya
uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
" Ujenzi wa Reli hii awamu ya kwanza
ulianzwa kupangwa na wajerumani ambao hawakuufanya, akaja Rais Hayati Benjamin
Mkapa na wengine waliofuata lakini aliyefanikiwa ni Dkt. Samia," alisema
Kadogosa.
Alisema katika kipindi cha miaka mitatu ya
uongozi wa Rais Dkt. Samia TRC imefanya mapinduzi mkubwa ya reli hapa nchini na
Afrika Mashariki kwa ujumla.
Alisema katika kipindi hicho, shirika hilo ambalo
limeundwa kupitia Sheria ya Reli Namba 10 ya Mwaka 2017 limefanikiwa kutekeleza
mradi wa ujenzi wa reli kwa sehemu tatu
lengo likiwa ni kutoa huduma ya usafirishaji wa abiria na mizigo na kusimamia
na kuendeleza miundombinu ya reli huku dhima ikiwa ni kusimamia usafiri wa reli
kwa kuendeleza miundombinu na kutoa huduma bora, endelevu na ya uhakika ya
usafiri.
Kadogosa alisema Serikali ilipata mkopo wa Dola
za Marekani milioni 300 kutoka Benki ya Dunia Machi 2014 kwa ajili ya
kutekeleza mradi wa kuboresha usafirishaji wa njia ya reli kati ya kipande cha Dar es Salaam hadi Isaka
chenye umbali wa kilometa 970.
Alisema katika kipindi hicho cha miaka mitatu ya
uongozi wa Rais Dkt.Samia shirika hilo limefanya kazi ya ukarabati wa mabehewa
na injini kwa ajili ya kuongeza vitendea kazi kwa lengo la kuongeza ufanisi na
kuboresha utendaji wa kazi.
Kadogosa alisema shirika limenunua mabehewa 22 ya
abiria, ukarabati wa mabehewa 37 ya abiria na 600 ya mizigo ambapo mabehewa 246
yamekarabatiwa na 24 ya abiria yamekarabatiwa hadi kufikia Disemba 2023.
Akizungumzia utekelezaji wa ujenzi wa kiwango cha
Standard Gauge alisema ujenzi huo umegawanyika katika awamu tatu ambapo awamu
ya kwanza ni kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza yenye jumla kilometa 1, 596 na
kipande cha Dar es Salaam- Morogoro cha
kilometa 300 na kipande cha Morogoro- Makutupora cha kilometa 422.
Alitaja vipande vingine kuwa ni kutoka
Makutupora- Tabora cha urefu wa kilometa 368 na Tabora Isaka cha kilometa 165
na kipande cha Isaka - Mwanza cha kilometa 341.
Aidha, Kadogosa akizungumzia miradi ya SGR
itakayotekelezwa kwa PPP aliitaja kuwa ni Mtwara- Mbamba Bay, Tanga -Arusha-
Musoma na kuwa Mtandao wa Reli ya Mijini itakuwa ni Dar es Salaam na Dodoma.
Kadogosa alisema fedha zilizotumika hadi sasa katika kutekeleza mradi huo ni Sh. Trilioni 23.3 na Sh. Trilioni 10.01 tayari amekwisha lipwa mkandarasi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kitengo cha Uhusiano TRC, Jamila Mbarouk alisema vyombo vya habari ni vya muhimu sana kwa ajili ya kufikisha taarifa kwa jamii na kuwa TRC inathamini mchango wa vyombo hivyo.
Naye Esther Zelemula ambaye ni Mhariri Mkuu wa Africa Media Group Limited akizungumza kwa ni haba ya Wahariri na Waandishi wa habari alisema jukumu kubwa la vyombo vya habari ni pamoja na kutangaza mafanikio mbalimbali yanayofanywa na Serkali pamoja na shirika hilo ili wananchi wayajue. Mhariri Mkuu wa Africa Media Group Limited , Esther Zelamula akitoa shukurani kwa niaba ya wanahabari wakati wa mkutano huo.Jarida la Reli na matukio mbalimbali likioneshwa baada ya kuzinduliwa rasmi. Kutoka kushoto ni Mhariri Mkuu wa Africa Media Group Limited , Esther Zelamula, Mkurugenzi Mkuu TRC, Masanja Kadogosa, Mhariri Msaidizi wa Gazeti la Nipashe, Epson Luago na Mkurugenzi wa Kitengo cha Uhusiano TRC, Jamila Mbarouk. Mkurugenzi wa Kitengo cha Uhusiano wa Shirika la Reli Tanzania (#TRC), Jamila Mbarouk akizungumza wakati wa mkutano huo.Waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo.Wahariri na Waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo.
No comments