MIAKA MITATU YA RAIS SAMIA YAPUNGUZA RUSHWA NCHINI
(MAKALA MAALUMU YA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA)
RUSHWA ni
tatizo la kidunia lenye madhara makubwa kwa mtu, jamii, nchi na mataifa kwa
ujumla. Rushwa imetumika kupoka haki za watu kwa kumnyanganya haki yeye
aliyeistahili na kumpa yule asiyeistahili kwa sababu mwenye jukumu la kutoa
haki amepokea hongo au kaahidiwa kupewa hongo ili apindishe sheria. Ni kwa
sababu ya rushwa wapo vijana wanaokosa fursa za masomo au za kupata mikopo ya
kibiashara na wengine kupendelewa na kupewa fursa hizo japo hawana sifa kwa
kuwa wametoa rushwa.
Mathalani,
taarifa ya utafiti uliofanywa na Transparency International ya mwaka 2023
kuhusu Corruption Perception Index (CPI) inaonesha kuwa Tanzania imefanya
vizuri na kupata alama 40 na kushika nafasi ya 87 kati ya nchi 180
zilizofanyiwa utafiti, ikilinganishwa na alama 38 ilizopata mwaka 2022 ambapo
ilishika nafasi ya 94. Tanzania, kwa mujibu wa taarifa hiyo, imeshika nafasi ya
pili katika mapambano dhidi ya rushwa katika ukanda wa Afrika Mashariki
ikitanguliwa na nchi ya Rwanda.
Kutokana na uwezeshaji wa TAKUKURU uliofanywa
na Serikali, kiasi cha Shilingi bilioni 201.72 imedhibitiwa na kurejeshwa
Serikalini kupitia operesheni mbalimbali za uchunguzi wa tuhuma za rushwa
pamoja na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo. Sehemu ya fedha hii imetumika
kutekeleza miradi mingine ya maendeleo kama vile ujenzi wa vituo vya afya,
manunuzi ya dawa na vifaa tiba pamoja na ujenzi wa shule na barabara ili kuleta
ustawi wa wananchi na maendeleo endelevu ya Taifa.
Vilevile, katika kipindi hiki cha miaka mitatu, uchunguzi wa
tuhuma za vitendo vya rushwa uliendelea na pale penye ushahidi na kwa kibali cha
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kesi zilifunguliwa na kuendeshwa mahakamani.
Jumla ya kesi 1,922 za rushwa ziliendeshwa mahakamani zikiwamo kesi 19
zilizofunguliwa katika Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ya
Mahakama Kuu ya Tanzania. Mahakama ilitoa maamuzi katika kesi 1,303 za rushwa
ambapo katika kesi 801 sawa na asilimia 61 Jamhuri ilishinda baada ya
washtakiwa kupatikana na hatia ya kutenda makosa ya rushwa na kuhukumiwa
kifungo jela au kulipa faini.
Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru CP. Salum Rashid Hamduni
Serikali pia imeiwezesha TAKUKURU kwa fedha ya
kuendelea kutekeleza jukumu lake la kuelimisha umma kuhusu madhara ya rushwa na
kuuhamasisha ushiriki katika mapambano dhidi ya adui rushwa. Hii ni sehemu ya
jitihada za kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa ambapo baadhi ya wadau
wamehamasika na kuchangia kuzuia vitendo vya rushwa kwa kuacha kushiriki
vitendo hivyo au kwa kutoa taarifa za vitendo vya rushwa huku wengine wakipata
ujasiri na kujitokeza kutoa ushahidi katika kesi za rushwa mahakamani.
Uelimishaji umma umefanyika kwa makundi mbalimbali katika jamii
kuanzia vijijini hadi mijini kupitia mikutano, minada, magulio, midahalo,
semina, warsha, mbio za Mwenge wa Uhuru, vipindi vya redio, vipindi vya
televisheni, na machapisho mbalimbali. Pia, elimu kwa umma imetolewa kupitia
maonesho ya kitaifa na kimataifa yanayofanyika kila mwaka nchini kama vile
maonesho ya Wakulima (Nanenane) na Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es
Salaam (Sabasaba).
Ili kuongeza ushiriki wa wadau katika kuzuia vitendo vya rushwa,
Programu ya TAKUKURU – Rafiki ilizinduliwa 20 Disemba, 2022. Programu hii
imelenga kushirikisha wadau kutatua kero katika utoaji wa huduma kwa umma na
utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambazo zikiachwa bila kutatuliwa zinaweza
kusababisha kutokea kwa vitendo vya rushwa. Utekelezaji wa Programu hii umekuwa
wenye mafanikio ambapo kero nyingi zilizoibuliwa zimetatuliwa hivyo kuzuia
vitendo vya rushwa na kuboresha huduma zinazotolewa kwa umma.
Katika hatua nyingine, mwaka 2023, Tanzania ilikuwa mwenyeji wa
Maadhimisho ya Siku ya Mapambano Dhidi ya Rushwa Barani Afrika yaliyofanyika
jijini Arusha kuanzia Julai 9-11, 2023. Hii ilikuwa heshima kubwa kwa Taifa na
inayoashiria imani ya Mataifa mengine ya Afrika pamoja na Umoja wa Afrika kwa
Tanzania katika suala la mapambano dhidi ya rushwa. Wadau mbalimbali wa
mapambano haya kutoka ndani na nje ya Tanzania wakiwemo kutoka sekta ya umma,
sekta binafsi na asasi za kiraia walishiriki maadhimisho hayo.
Akihutubia wadau hao siku ya kilele Julai 11, 2023, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia pamoja na mambo mengine
aliwatahadharisha watu wanaojihusisha na rushwa kuhusu mienendo yao.
“Walarushwa wanapaswa kufahamu kuwa nchi zetu si vichaka vya kuficha fedha
zilizotokana na rushwa au kufuga walarushwa. Tunataka dunia nzima ifahamu kuwa,
Afrika si salama kwa walarushwa na hilo lionekane kwa vitendo kupitia hatua
tunazozichukua dhidi ya walarushwa”, alisisitiza Rais Samia.
Mheshimiwa Rais Samia hakuishia kutoa onyo hilo bali aliueleza
ulimwengu mafanikio ya hatua zilizochukuliwa na Tanzania kuidhibiti rushwa,
yaani kazi zilizofanyika kuzuia na kupambana na rushwa. Mathalani, alisema kuwa
katika kipindi cha miaka mitatu, kupitia mapambano dhidi ya rushwa Serikali
iliokoa zaidi ya Shilingi bilioni 139 ya fedha ya umma. Fedha hizo ukinipa mimi
sasa hivi nikifumba macho nakwambia nazipeleka kununua vifaa tiba, alisema Mhe.
Dkt. Samia.
Rais Samia aliwaomba viongozi barani Afrika kushirikiana katika
kupambana na vitendo vya rushwa na kusisitiza kuwa moja ya vikwazo vikubwa vya
maendeleo barani Afrika ni janga la rushwa ambalo linadhoofisha mifumo ya kitaasisi
na kuathiri mipango na mikakati ya kujikomboa kiuchumi. Pia, alitumia jukwaa la
maadhimisho hayo, pamoja na mambo mengine, kumtaka kila Mtanzania kujitathmini
ni kwa namna gani anadhibiti rushwa huku akiirejea kaulimbiu ya TAKUKURU.
‘‘Kuzuia Rushwa ni Jukumu Lako na Langu ; Tutimize Wajibu Wetu. Ni
kaulimbiu nzito na kaulimbiu inayotupa mtihani hasa sisi Watanzania, tujitizame
sisi wenyewe mmojammoja, tunaendana na kaulimbiu hii ? alihoji Rais Samia.
”Nitasimama imara kwenye mapambano dhidi ya rushwa” hii ni ahadi
aliyoitoa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania wakati anapokea taarifa ya utendaji kazi wa TAKUKURU Machi 28, 2021
katika Ikulu ya Chamwino ikiwa ni siku tisa tangu ale kiapo cha kuwa Rais.
Tunawiwa kusema, ahadi hii ameitekeleza kwa vitendo na Watanzania hatuna budi
kusimama imara na kuungana naye kwenye mapambano haya kwa kuizingatia kaulimbiu
”Kuzuia Rushwa ni Jukumu Lako na Langu; Tutimize Wajibu Wetu.”
Mathalani, taarifa ya utafiti uliofanywa na Transparency
International ya mwaka 2023 kuhusu Corruption Perception Index (CPI) inaonesha
kuwa Tanzania imefanya vizuri na kupata alama 40 na kushika nafasi ya 87 kati
ya nchi 180 zilizofanyiwa utafiti, ikilinganishwa na alama 38 ilizopata mwaka
2022 ambapo ilishika nafasi ya 94. Tanzania, kwa mujibu wa taarifa hiyo,
imeshika nafasi ya pili katika mapambano dhidi ya rushwa katika ukanda wa
Afrika Mashariki ikitanguliwa na nchi ya Rwanda.
Aidha, ili kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa hivyo kuhakikisha
ustawi wa umma, Serikali imefanya maboresho ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa, Sura 329 ili iendane na mazingira ya sasa ya kiuchumi, kijamii na
kiteknolojia. Muswada wa maboresho hayo ya Sheria upo katika hatua ya
kuwasilishwa Bungeni. Hii ni hatua muhimu katika mapambano haya.
Pia, Serikali imeimarisha uwezo wa kiutendaji wa Taasisi ya Kuzuia
na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa kuiwezesha kwa rasilimali watu,
rasilimali fedha, vitendea kazi pamoja na mafunzo ya weledi kwa watumishi.
Mapema mwaka huu 2024, Serikali imetoa kibali cha ajira za watumishi 350 hivyo
kufanya idadi ya watumishi wapya wa TAKUKURU katika kipindi cha miaka mitatu ya
uongozi wa Rais Samia kufikia 880. Uimarishaji huu wa TAKUKURU umeifanya
kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi hivyo kuimarisha mapambano dhidi ya
rushwa nchini.
Kutokana na uwezeshaji wa TAKUKURU uliofanywa
na Serikali, kiasi cha Shilingi bilioni 201.72 imedhibitiwa na kurejeshwa
Serikalini kupitia operesheni mbalimbali za uchunguzi wa tuhuma za rushwa
pamoja na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo. Sehemu ya fedha hii imetumika
kutekeleza miradi mingine ya maendeleo kama vile ujenzi wa vituo vya afya,
manunuzi ya dawa na vifaa tiba pamoja na ujenzi wa shule na barabara ili kuleta
ustawi wa wananchi na maendeleo endelevu ya Taifa.
Serikali pia imetaifisha mali zenye thamani ya Shilingi bilioni
2.14 zikijumuisha nyumba, viwanja na magari. Aidha, miradi ya maendeleo 3,576
yenye thamani ya Shilingi trilioni 16.76 ilifuatiliwa kwa madhumuni ya
kuhakikisha kuwa fedha hiyo inatumika kadiri ilivyokusudiwa ili kuwaletea
wananchi maendeleo.
Vilevile, katika kipindi hiki cha miaka mitatu, uchunguzi wa
tuhuma za vitendo vya rushwa uliendelea na pale penye ushahidi na kwa kibali
cha Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kesi zilifunguliwa na kuendeshwa mahakamani.
Jumla ya kesi 1,922 za rushwa ziliendeshwa mahakamani zikiwamo kesi 19
zilizofunguliwa katika Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ya
Mahakama Kuu ya Tanzania. Mahakama ilitoa maamuzi katika kesi 1,303 za rushwa
ambapo katika kesi 801 sawa na asilimia 61 Jamhuri ilishinda baada ya
washtakiwa kupatikana na hatia ya kutenda makosa ya rushwa na kuhukumiwa
kifungo jela au kulipa faini.
Serikali pia imeiwezesha TAKUKURU kwa fedha ya
kuendelea kutekeleza jukumu lake la kuelimisha umma kuhusu madhara ya rushwa na
kuuhamasisha ushiriki katika mapambano dhidi ya adui rushwa. Hii ni sehemu ya
jitihada za kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa ambapo baadhi ya wadau
wamehamasika na kuchangia kuzuia vitendo vya rushwa kwa kuacha kushiriki
vitendo hivyo au kwa kutoa taarifa za vitendo vya rushwa huku wengine wakipata
ujasiri na kujitokeza kutoa ushahidi katika kesi za rushwa mahakamani.
Uelimishaji umma umefanyika kwa makundi mbalimbali katika jamii
kuanzia vijijini hadi mijini kupitia mikutano, minada, magulio, midahalo,
semina, warsha, mbio za Mwenge wa Uhuru, vipindi vya redio, vipindi vya
televisheni, na machapisho mbalimbali. Pia, elimu kwa umma imetolewa kupitia
maonesho ya kitaifa na kimataifa yanayofanyika kila mwaka nchini kama vile
maonesho ya Wakulima (Nanenane) na Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es
Salaam (Sabasaba).
Ili kuongeza ushiriki wa wadau katika kuzuia vitendo vya rushwa,
Programu ya TAKUKURU – Rafiki ilizinduliwa 20 Disemba, 2022. Programu hii
imelenga kushirikisha wadau kutatua kero katika utoaji wa huduma kwa umma na
utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambazo zikiachwa bila kutatuliwa zinaweza
kusababisha kutokea kwa vitendo vya rushwa. Utekelezaji wa Programu hii umekuwa
wenye mafanikio ambapo kero nyingi zilizoibuliwa zimetatuliwa hivyo kuzuia
vitendo vya rushwa na kuboresha huduma zinazotolewa kwa umma.
Katika hatua nyingine, mwaka 2023, Tanzania ilikuwa mwenyeji wa
Maadhimisho ya Siku ya Mapambano Dhidi ya Rushwa Barani Afrika yaliyofanyika
jijini Arusha kuanzia Julai 9-11, 2023. Hii ilikuwa heshima kubwa kwa Taifa na
inayoashiria imani ya Mataifa mengine ya Afrika pamoja na Umoja wa Afrika kwa
Tanzania katika suala la mapambano dhidi ya rushwa. Wadau mbalimbali wa
mapambano haya kutoka ndani na nje ya Tanzania wakiwemo kutoka sekta ya umma,
sekta binafsi na asasi za kiraia walishiriki maadhimisho hayo.
Akihutubia wadau hao siku ya kilele Julai 11, 2023, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia pamoja na mambo mengine
aliwatahadharisha watu wanaojihusisha na rushwa kuhusu mienendo yao. “Walarushwa
wanapaswa kufahamu kuwa nchi zetu si vichaka vya kuficha fedha zilizotokana na
rushwa au kufuga walarushwa. Tunataka dunia nzima ifahamu kuwa, Afrika si
salama kwa walarushwa na hilo lionekane kwa vitendo kupitia hatua
tunazozichukua dhidi ya walarushwa”, alisisitiza Rais Samia.
Mheshimiwa Rais Samia hakuishia kutoa onyo hilo bali aliueleza
ulimwengu mafanikio ya hatua zilizochukuliwa na Tanzania kuidhibiti rushwa,
yaani kazi zilizofanyika kuzuia na kupambana na rushwa. Mathalani, alisema kuwa
katika kipindi cha miaka mitatu, kupitia mapambano dhidi ya rushwa Serikali
iliokoa zaidi ya Shilingi bilioni 139 ya fedha ya umma. Fedha hizo ukinipa mimi
sasa hivi nikifumba macho nakwambia nazipeleka kununua vifaa tiba, alisema Mhe.
Dkt. Samia.
Rais Samia aliwaomba viongozi barani Afrika kushirikiana katika
kupambana na vitendo vya rushwa na kusisitiza kuwa moja ya vikwazo vikubwa vya
maendeleo barani Afrika ni janga la rushwa ambalo linadhoofisha mifumo ya
kitaasisi na kuathiri mipango na mikakati ya kujikomboa kiuchumi. Pia, alitumia
jukwaa la maadhimisho hayo, pamoja na mambo mengine, kumtaka kila Mtanzania
kujitathmini ni kwa namna gani anadhibiti rushwa huku akiirejea kaulimbiu ya
TAKUKURU. ‘‘Kuzuia Rushwa ni Jukumu Lako na Langu ; Tutimize Wajibu Wetu.
Ni kaulimbiu nzito na kaulimbiu inayotupa mtihani hasa sisi Watanzania,
tujitizame sisi wenyewe mmojammoja, tunaendana na kaulimbiu hii ? alihoji
Rais Samia.

No comments