RC HALIMA DENDEGO KARIBU SINGIDA KUONGEZA KASI YA MAENDELEO YA RAIS SAMIA
Na Dotto Mwaibale, Singidani Blog.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuboresha utendaji kazi
wa Serikali amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa,
Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya na wengine kuhamishiwa
katika vituo vingine vya kazi.
Kwa Mkoa wa Singida katika mabadiliko hayo aliyekuwa mkuu wa mkoa huo Peter
Serukamba amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa
Irinda Halima Dendego amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Katika nafasi ya Wakuu wa Wilaya waliopata uhamisho ni aliyekuwa Mkuu wa
Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskas Muragili ambaye amehamishiwa Wilaya ya
Bukombe huku aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Godwin Gondwe akihamishiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Singida.
Kwa upande wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya aliyekuwa Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Jimson Mhagama amehamishiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Same na Annastazia Ruhamvya
aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same kuhamishiwa Wilaya ya
Manyoni.
Aidha, aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, John Mgalula
amehamishiwa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi na nafasi yake kuchukuliwa na
Ayubu Kambi aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga.
Bodi ya Wakurugenzi ya Blog ya Singidani inatoa pongezi kwa Mhe. Halima Omary Dendego kwa kuwa Mkuu wa Mkoa mpya wa Singida na kuwa kiongozi wa wasaidizi wake wote. Bodi hiyo inawakaribisha Singida na kuwa itaendelea kuwapa ushirikiano mkubwa wa kuandika habari za maendeleo ili kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan kuongeza kasi ya kuinua uchumi wa wana Singida na nchi kwa ujumla kama ilivyokuwa ikifanya kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba ambaye amehamishiwa Mkoa wa Iringa.
No comments