FALSAFA YA 4R YAMPATIA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, SHAHADA NYINGINE YA UDAKTARI
*Falsafa ya 4R yampatia Rais Samia shahada nyingine ya udaktari
*Baada ya India, chuo kingine kikuu kikubwa cha Uturuki chamtunuku Rais Samia shahada ya udaktari
................................
Na Mwandishi Wetu - Zanzibar
Huku wakiwa wameshika bango lenye kauli mbiu
maarufu ya "Songa na Samia," vijana wanaopiga mbizi kwa sarakasi
kwenye eneo la Forodhani la Zanzibar, wametoa video yao mpya kuchambua falsafa
ya 4R ya Rais Samia Suluhu Hassan kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano
wa Tanganyika na Zanzibar.
Siku chache baada ya vijana hao kutoa video yao
hiyo, Rais Samia ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (Honoris Causa) ya
Uchumi na Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki kwenye hafla iliyofanyika chuoni
hapo Ankara, Uturuki, leo tarehe 18 Aprili, 2024.
Mwezi Oktoba mwaka jana, Rais Samia alitunukiwa
shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa ya kielimu (Doctorate Honoris Causa)
na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru nchini India. huku akiendelea na ziara yake
nchini India.
Hadi sasa, Rais Samia ametunukiwa shahada za
heshima takribani 4 kutoka vyuo vikuu vikubwa ndani ya nje ya nchi ndani ya
miaka mitatu tu ya Urais wake.
Shahada hizo zinatambua jitihada kubwa
inayofanywa na Serikali yake kuleta mabadiliko katika mifumo ya kisiasa,
kiuchumi na katika sheria zetu za uchaguzi nchini.
Kwenye uongozi wake, Rais Samia anaamini katika
kile kinachojulikana kama 4R – ikiwa ni ufupisho wa maneno manne ya lugha ya
Kiingereza; Reconcilation (Maridhiano), Resilience (Ustahamiliivu), Reforms
(Mabadiliko) na Rebuidlding (Kujanga Upya).
Hizi ndiyo 4R za Rais Samia ambazo zimeleta
mafanikio makubwa kwenye uongozi wake tangu aingie madarakani Machi 19, 2021:
MARIDHIANO
Kwenye kujenga Tanzania bora,.Rais Samia amesema
kuwa anatamani kujenga jamii yenye maridhiano na maelewano. Anatamani kujenga
umoja pasipo kujali tofauti zetu za kisiasa, kidini, kikabila na nyingine zote.
Hili litawezekana kwa kujenga jamii inayopata
haki sawa mbele ya sheria, isiyobaguana
na inayotoa fursa sawa sawa za kiuchumi kwa wote.
Rais Samia anaamini kuwa maridhiano hayawezi
kupatikana penye ubaguzi na pale ambapo kuna wanaokosa fursa na haki zao za
kiuchumi na kiraia.
USTAHIMILIVU
Tanzania haiwezi kusonga mbele kama wananchi na
viongozi watakuwa legelege kulinda yaliyo yetu. Wahenga walisema Umoja ni Nguvu
na namna pekee ya kupambana na changamoto zote zinazoikumba dunia kwa sasa ni
kwetu sisi kufanya hivyo kwa Umoja na Mshikamano.
Huko tuendako tutatikiswa na kuyumbishwa. Iwe
kiuchumi, kimazingira, kijamii na kisiasa lakini ni lazima tujenge
ustahamivu," Rais Samia alisema.
Hii ni kwa sababu hakuna nchi nyingine zaidi ya
hii na hapa ndiyo kwetu. Nilitiwa nguvu sana na namna Watanzania walivyopokea
tukio la Royal Tour kwa uzalendo wa kipekee.
MABADILIKO
Kuna msemo mmoja maarufu kwamba kitu pekee cha
uhakika kwa mwanadamu ni mabadiliko.
Rais Samia amedhamiria kwamba serikali yake
itajitahidi kufanya mabadiliko katika mifumo ya kisiasa, kiuchumi na katika
sheria zetu za uchaguzi.
Lengo ni kwamba Tanzania iende na wakati na –
kama ilivyokuwa wakati mwingine, tujue mapema ni wakati gani wa kufanya jambo
hata kama si watu wanaliunga au hawaliungi mkono kwa wakati husika.
Mabadiliko katika sheria za uchaguzi yataleta
ushindani wa haki na kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao kuwaongoza.
Kwenye uchumi, mabadiliko yatakuwa na lengo la kutoa fursa zaidi kwa watu wengi
zaidi kunufaika kiuchumi badala ya wachache.
KUJENGA UPYA
"Ninafahamu kwamba wananchi hawali
maridhiano, ustahamivu wala mabadiliko," Rais Samia alisema.
Kama walivyofanya watangulizi wa Rais Samia,
lengo kuu linatakiwa kuwa ukuaji wa uchumi wa Tanzania. Uchumi utakaoongeza
ajira kwa vijana wetu na utakaofungua fursa kwa makundi yote ya kijamii yaliyo
nchini.
Tayari serikali inaendeleza miradi mikubwa ya
miundombinu na mengine kwenye sekta ya madini na nishati. Juhudi zilizofanywa
kupitia kampeni ya Royal Tour zina lengo la kuzimua sekta muhimu ya utalii
iliyoathiriwa sana na ugonjwa wa Covid 19. Katika kilimo serikali inafanya
mabadiliko makubwa ili sekta hiyo muhimu ianze kuwa na mchango inaostahili
kwenye uchumi wetu.
"Ninaamini kwamba kwa jitihada zetu za R nne, tutaweza kutimiza malengo ya kuwa na mfumo wa vyama vingi vya siasa. Lengo kuu halikuwa kuwa na vyama vingi vya siasa bali lengo lilikuwa kujenga jamii yenye uzalendo, maridhiano, ustahamivu na yenye uchumi unaokua kwa wote na endelevu," Rais Samia alisema.
No comments