KATIBU TAWALA WILAYA YA MISUNGWI AUNGANA NA WANANCHI KULIOMBEA TAIFA
........................
Na King Bashite, Misungwi
KATIBU Tawala Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Abdi Makange ameongoza mamia ya wananchi wa Misungwi kuliombea Taifa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan mapema asubuhi ya leo Aprili 22, 2024 Uwanja wa Aman mjini Misungwi.
Katika maombi hayo maalumu Makange aliwaalika viongozi wa dini zote na madhehebu mbalimbali wilayani Misungwi yenye lengo la kuliombea Taifa na viongozi wote wa serikali.
Akizungumza wakatai wa maombi hayo Makange alisema sherehe jizo ambazo zimeambatana na maombi hayo zimeanza leo wilayani humo ikiwa ni mwendelezo wa kusherekea miaka 60 ya kuadhimisha kumbukuzi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo ilizaliwa Tanzania.
Alisema sherehe hizo zinaendelea hadi siku ya kilele cha maadhimidho hayo Aprili 26, 2024 ambapo zitafanyika shughuli za kijamii kama upandaji wa miti na mambo mengine.
Makange alitumia nafasi hiyo kuzipongeza Serikali zote mbili kwa kuulinda muungano na kuendelea kuondoa kero na changamoto zinazojitokeza kwa ajil9i ya kuhuimarisha.
Aidha, Makange amewashukuru viongozi wote wa dini, Kamati ya Amani ya Wilaya ya Misungwi kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika mambo mbalimbali.
No comments