WAZIRI MKUU KUSHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA 20 YA MIRADI YA UMWAGILIAJI
.....................
NIRC Dodoma.
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa
mgeni rasmi katika utiaji saini mikataba 20 ya ukarabati na ujenzi wa miradi ya
umwagiliaji baina ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji chini ya Wizara ya Kilimo na
Wakandarasi jijini Dodoma hapo kesho.
Mikataba hiyo ni ya ujenzi na ukarabati wa Skimu
14 pamoja na miradi sita (6) ya usanifu wa kina na upembuzi yakinifu ili
kampuni zilizoshinda zabuni ziweze kuanza zoezi la utekelezaji wa miradi hiyo
kupitia mikataba husika.
Baadhi ya miradi hiyo ni pamoja na skimu ya Itping
iliyopo wilaya ya Njombe mkoani Njombe, Skimu ya Mahiga iliyopo wilaya ya
Kwimba mkoani Mwanza, Skimu ya Msange iliyopo Wilaya ya Singida mkoani Singida,
Skimu za Ndungu na Kihurio zilizopo Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, ujenzi
wa Bwawa na Skimu ya Luiche katika Wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma.
Kwa upande wa usanifu wa kina na upembuzi yakinifu katika Bwawa la Kalupale lililoko Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora, upembuzi yakinifu katika Skimu ya Ifakara - Idete iliyopo Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro, eneo lingine ni Pamoja na Skimu ya Butonga – Nyamazuka, Igaka – Bundala na Isole mkoani Mwanza.
No comments