NEEC KUPITIA PROGRAMU YA IMASA KUWAWEZESHA WANAWAKE DAR ES SALAAM WATAKAO JIIBULIA FURSA ZA BIASHARA
...............................
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BARAZA la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limewataka akinamama
wa Mkoa wa Dar es Salaam kutumia fursa za kibiashara zinazopatikana katika Mkoa
huo ili kuanzisha shughuli za ujasiriamali na biashara ili kuleta matokeo
chanya kwenye Familia zao na Taifa kwa ujumla.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, RC Albert Chalamila wakati
wa uzinduzi wa Programu ya Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA) katika Mkoa
huo ambapo alisema kwamba kuna umuhimu kwamba wakinamama wachukue changamoto na
matatizo mbalimbali kama fursa za kuweza kuinuka kiuchumi.
Alisema kwamba Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amekuja na programu hii
ili kumuwezesha mwanamke wa nchini kutoka kwenye lindi la umasikini na
anaendelea kushughulikia na mikopo ya wanawake na watu kwenye makundi maalum
ili iende kwa walengwa.
“Juhudi za kila siku za shughuli za kijasiriamali ndio zitakazotutoa
kimaisha na kuendelea kuchangamkia fursa za kiuchumi,” alisisitiza
Alisema hayo jana katika unzinduzi wa program ya Imarisha Uchumi na Mama
Samia (IMASA) inayotekelezwa na baraza hilo ambapo prongram ilizinduliwa kwa
mkoa wa Dar es Salaam.
Tunampongeza Rais Mama Samia kwa kutuletea program hii Imarisha Uchumi na
Mama Samia katika mkoa wetu, na sisi tumeipokea program hii kwa mikono miwili,
na tunalenga kutekeleza kwa vitendo na lengo letu azma hiyo iweze kutimia.
Alisema Mkoa wa Dr es Salaam unafursa nyingi zikiwemo za kilimo cha
mbogamboga, ufugaji wa kuku, Samaki ni kwenye mabwawa ya kuchimba.
“kwa sasa mkoa huu unajipanga kuendelea kujenga masoko makubwa ya kisasa
katika kila wilaya nak ama mnavyojua kwamba soko la Kariakoo linajengwa la
kisasa zaidi na lipo katika hatua za mwisho,’ alisema RC Chalamila
Aliongeza kwamba Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ana ndoto za
kuwawezesha wanawake wa nchini kiuchumia kwa kutaka kuwaunganisha na biashara
na fursa zitokanazo na miradi ya kimkakati unayoendelea hapa nchini.
Alisema kwamba serikali ya Mkoa itaendelea kuwahamasisha wakinamama katika
juhudi za kutaka wajihusishe na shughuli za ujasiriamali kwa kutumia fursa
zilizopo za miundombinu ya reli, Barabara na kiwanja cha ndege kwa ajili ya
usafirishaji wa bidhaa mbalimbali.
Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Beng`i Issa alisema baraza
lake kupitia programa ya Imarisha Uchumi na Mama Samia imekuja kuwakwamua
wanawake, vijana na makundi maalumu kufanya shughuli za kijasiriamali.
`Baraza la linatambua Mkoa wa Dar es Salaam mkoa unahitaji maeneo kwa ajili
ya kusindika mazao yao, kuwa na masoko (super market) ili wateja waweze kwenda
kununua bidhaa zilizotengenezwa hapa nchini.
Alisema baraza limejipanga kuwaunganisha wanawake na taasisi mbalimbali
ikiwemo ya Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) pamoja na Shirika la Viwango
Tanzania (TBS) ili kupata technolojia na vibali mbalimbali.
Alifafanua kwamba baraza linaprogram mbalimbali ikiwemo ya local content
ili watanzania waweze kushiriki katika miradi mikubwa kama ya SGR, bomba la
mafuta.
Programa nyingine nyingine ni ya ufundishaji somo la ujasiriamali kuanzia
shule ya msingi hadi vyuo vikuu lengo ni kuwaandaa watanzania kuwa wajasirimali
na kuchangia uchumi wa taifa.
Vilevile aliwataka wanawake wa mkoa wa Dar es Salaam kuwa na nidhamu ya
fedha kwa kuweka katika akaunti au katika vibubu ili kuendeleza biashara
zao.
Jiungeni katika vikundi vya VICOBA ili kusaidia kuweka fedha na kukopa kwa
vile mnakopeshana kwa riba nafuu na kujiepusha na ukoaji katika vikundi vya
kausha damu.
Serikali ina mifuko mbalimbali ya uwezeshaji mikopo lakini ili kupata
mwanahitajika kufuata masharti kupata fedha hivyo kila mmoja anahitajika
kukidhi vigezo na kutunza kumbikumbu ili kupata fedha.
Bi Issa alisema kwamba programu hiyo ya Imasa moja ya jukumu lao ni kupitia program ya IMASA kuwezesha wanawake wa Dar es Salaam watakaojiibulia fursa za kibiashara.Mshauri wa Rais katika mambo ya Wanawake na Makundi Maalum, B.Sophia Mjema akiteta Jambo na Katibu wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi Beng'i Issa wakati wa Uzinduzi wa Program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia kwa Mkoa wa Dar es Salaam.Katibu wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi Beng'i Issa (kulia) akiserebuka na viongozi wengine wakati wa uzinduzi wa Program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia kwa Mkoa wa Dar es Salaam. Katikati mwenye kilemba (cheupe) ni Mshauri wa Rais katika mambo ya Wanawake na Makundi Maalum, Bi.Sophia Mjema. Wengine ni makundi ya Wanawake.
No comments