IMASA IMEUNDWA KWA LENGO LA KUHIMARISHA BIASHARA NA SIO KUGAWA FEDHA
..............................
Na Mwandishi Wetu, Iringa
Baraza la Uwzeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limeyataka makundi ya kinamama, vijana na makundi maalumu kutambua kuwa Program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA) imeanzishwa ili kuongoza tija kwa wafanyabiahara na wajasiriamali wenye biashara zao na siyo kuwa imekuja kutoa fedha kwa makundi hayo.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Bi. Beng’i Issa wakati alipokuwa akizungumza na makundi hayo katika Mkoa wa Iringa kuwa program hiyo haijaanzishwa kwa ajili ya kutoa fedha kwa makundi hayo bali kuleta uwezeshaji kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wenye biashara zao.
“Program hii ya Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA)inajieleza vizuri kuwa imekuja kuimarisha biashara zilizopo ili kuwa na tija,” Uwezeshaji huo ni kwa ajili ya biashara ambazo zinafanyika na siyo kutoa fedha, alifafanua, Bi. Beng’i.
Akitoa mafano alisema kwamba program hiyo itawaimarisha wafanyabiashara kwa kibiashara wanazofanya, wakulima katika kilimo wanachofanya, kadhalika katika uvuvi na ufugaji. Pia uwezeshaji huo utaangalia vipaumbele vilivyopo katika mkoa husika na kutoa vitendea kama mashine, viwanda na vilevile ujuzi.
Bi, Beng’I alisema kwamba suala la mitaji litaangaliwa lakini kipaumbele kikubwa cha program hiyo ni kutoa vitendea kazi kwa ajili ya kuimarisha shughuli hizo za biashara na ujasiriamali. Makundi hayo kwa Mkoa huo wengi wanafanya shughuli za kilimo na ufugaji na baraza limeona shughuli hizo na ndio zitakazokuwa za kipaumbele.
Pia alisema wafanyabiashara wengine katika mkoa huo wanafanya shughuli za kusindika mazao ya kilimo na mifugo, na baraza kupitia madawati yake ya wilaya na mikoa yatatoa elimu namna ya kutumia mitandao ya teknonolojia waweze kufanya manunuzi ya umma kupitia mitandao kwa lengo la kupata fursa zilizopo serikali,
Mshauri wa Rais Masuala ya Wanawake, Sophia, Mjema alisema serikali imejiwekeza katika kuhakikisha shughuli za kiuchumi zinawezeshwa na aliwataka makundi hayo kujiandikisha na kutambuliwa pamoja na biashara zao ili kuweza kupata uwezeshaji.
“ Kutokana na shughuli kubwa za kilimo kama cha maua, miti ya mbao tunahitaji hapa muwe na kiwanda kikubwa cha kuchakata mazao haya”, na aliwataka viongozi wa mkoa huo kuwapa kazi za shughuli ndogondogo za ujenzi wapewe makundi hayo ili wawe wakandarasi wadogo.
Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wilaya ya Mfindi, Bi.Pascazia Lutu alisema elimu waliyoipata wataenda kuitumia na kuelimisha wengi ili waweze kuwa na mabadiliko ya kiuchumi.
Naye Mwananchi kutokana Manispaa ya Iringa, Bi. Mahanga Mng’ong’o alipongeeza mpango wa serikali wa kuwezesha makundi ya akinamama na hiyo itasaidia kujiepusha na mikopo toka katika taasisi mbalimbali zikiwemo kausha damu.
“ Hapa nimeona pia kunamikopo
katika Benki ikiwemo NMB na hata katika halmashauri hivyo tumenufaika na elimu
ambayo tumeipata hapa,” kumwezesha mama ni kuiwezesha familia nzima, alisisitiza.
Mshauri wa Rais Masuala ya wanawake, Bi. Sophia Mjema wa pili kutoka kulia akifuatilia jambo kutoka kwa makundi ya akinamama, vijana na makundi maalumu hawako pichani Mkoani Iringa wakati Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) lilopoifikisha programa ya Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA)mkoani humo, wa kwanza kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Bi.Beng’I Issa, wa pili kutoka kushoto ni Rais Mkoa wa Iringa Doris Kalasa na wa kwanza kulia ni Bi. Rita Mlagala. Picha na Mwandishi Wetu Iringa.
No comments