NEEC YASHAURI MAKUNDI YA KINAMAMA YAJIANDAE KUFANYA BIASHARA NA VIWANDA NA MIRADI YA SERIKALI
Matibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa akizungungumza na Makundi ya Kinamama, Vijana na Makundi Maalumu wakati baraza hilo lilipoifikisha program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA)
Na Mwandishi, Wetu Mtwara
Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiunchumi (NEEC) kupitia
program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA) limeyashauri makundi ya
kinamama, vijana na makundi maalumu Mkoaani Mtwara kujisajili kupata sifa ya kufanya biashara na viwanda
vikubwa na miradi mbalimbali ya serikali ili kuondokana na hali duni ya vipato na kushiriki katika
uchumi wa taifa
Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Bi. Beng”i Issa alitoa ushuri
huo kwa makundi hayo jana wakati baraza hilo lilipoifikisha programa ya IMASA
katika Mkoa wa Mtwarwa kuwa makundi hayo yanahitajika kujisajili na kukidhi vigezo
ili yaweze kuunganishwa kufanya biashara na viwanda vikubwa na miradi mbalimbali
ya serikali kwa nia ya kuondokana na vipato duni na kushiriki katika uchumi wa
taifa.
“Mkoa huu wa Mtwara unafursa ya uwepo wa viwanda vikubwa na
miradi mbalimbali ya serikali inayotekelezwa na inayokuja mtaunganishwa nayo
kibiashara ili mshiriki katika uchumi wa taifa,” na hii ndiyo kazi ya baraza ya
uwezeshaji wananchi kiuchumi, alisema Bi. Beng”i.
Alisema katika mkoa wa Mtwara kunamiradi inakuja ikiwemo ya gesi,
upanuzi wa uwanja wa ndege na bandari hivyo makundi hayo au wafanyabiashara watahitajika
kutoa huduma za bidhaa kama za saruji, changa, kokoto, na hata chakula, shughuli
za ulinzi na usafi.
Akifafanua zaidi alisema uwekezaji unaofanywa na wageni au
wafanyabiahara wa ndani lazima kuwe na mpango wa kushirikisha watanzania kupata
ajira za ujuzi na zisizo za ujuzi na kutoa huduma mbalimbali.
Bi, Beng”I alisema ili kupata fursa hizo wanahitajika
kujipanga kuwa katika vikundi hivyo au mtu mmojamoja na kusajiliwa, kuwa na
vitambulisho vya NIDA, akaunti benki, kuwa na biashara na mitaji na hiyo itasaidia kupata takwimu
halisi na kupanga vipaumbele vya mkoa
Alisema program hiyo ya IMASA inaawamu mbili ya kwanza kupata
taarifa na kutengeneza kanzidata na awamu ya pili ni ya kutoa uwezeshaji na progrwamu
hiyo ni kwa nchi nzima.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bw. Patrick Sawala alisema wamepokea
programa ya IMASA na kuitekleza pamoja na watalaam kuhakikisha wananchi
wanatumia fursa hiyo kushiriki katika uchumi wa taiafa lao.
“Tumeletea program na nawaomba wananchi watumie fursa za kilimo,
ufugaji, uvuvi na usindikaji wa mazo,” na aliongeza kusema pia mkoa huo kuna
kilimo cha mwani, ufugaji wa majongoo, utalii wa kitamaduni na kutembelea mbuga.
Alisema ,mkoa wake vijiji na vitongoji vyote vinatarajia
kupata nishati ya umeme ambyo itakuwa chachu ya kuanzisha viwanda vidogo na
biashara kusaidia kukuza vipatoa kwa wananchi.
Naye wananchi Bi. Khadija Mela alisema amepata elimu kuwa
aliyeanza biashara aendelee na wasionabiashara wajiunge katika vikundi au mtu
mmojammoja ili kupata uwezeshaji.
“watu ambao hawajafika kupata elimu hii wakisikia tena wafike
lakini na sisi tunaenda kuwa mabalozi kwa vile ni program inayolenga kutukomboa
kiuchumi akinamama,”alisema.
Kwa Upande wake Fadhili Ngavuja alisema anashukuru program nia ya kutaka kuwakwamua mkundi hayo na yeye amejiunga kwa ajili ya kuingia katika kanzidata ya baraza ili kupata uwezeshaji na anataraji atakuwa kijana mpya na kushiriki kukuza uchumi.
Makundi ya Kinamama, Vijana na Makundi Maalumu wa Mkowa Mtwara wakipata mafunzo ya ujasiriamali wakati Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) lilipoifikisha program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA) mkowani Mtwara.
No comments