WAZIRI MKUU AZINDUA KITUO CHA UWEKEZAJI WANANCHI KIUCHUMI NYANG"WALE MKOANI GEITA
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akivuta pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi katika
Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Nyang’wale kuwa kitu hicho kimezinduliwa,
kituo hicho ni cha Baraza la Uwezeshaji Kiuchumi (NEEC), kulia ni Katibu
Mtendaji wa Baraza hilo, Bi. Beng’i Isssa,kulia ambaye haonekani vizuri ni mkuu
wa mkoa wa Geita Martin Shigela na wapili kutoka kulia ni Naibu Waziri Sera
Bunge na Uratibu Ummy Nderiananga. Picha na Mwandishi wetu, Nyang’wale Geita.
.................................
Na Mwandishi Wetu, Geita
WANANCHI wa Wilaya ya Nywang’wale Mkoani Geita wametakiwa
kukitumia Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kilichojengwa wilayani kwao kuanzisha shughuli za biashara
na ujasiriamali ili kuwasaidia kuwa na vipato na kushiriki katika Uchumi wa
taifa lao
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati
alipokuwa akizindua Kituo hicho ambacho ni kituo cha Baraza la Uwezeshaji
Wananchi (NEEC), ambacho kitafanya kazi ya kuwasaidia wananchi kupata huduma
mbalimbali za uwezeshaji kushiriki
katika Uchumi wa nchi.
“Wilaya hii imejaliwa kuwa na fursa nyingi ikiwemo ya kilimo,
ufugaji, madini hivyo kituo hiki kimejengwa kwa nia ya kuwaletea huduma karibu,”
huduma zitakazotolewa ni Pamoja na elimu ya ujasiriamali, urasimishaji wa biashara
na kupata mikopo nafuu, alifafanua.
Alisema kwa sasa hakunasababu ya wananchi kulalamikia mitaji
kwa vile serikali imewaletea jengo hilo na mikopo itapatikana hapo na kwenye
halmashauri bali wao kuchangamkia fursa hiyo.
Hatahivyo asisitiza kwamba wakifanikiwa kupata mikopo hiyo
inayotolewa katika jengo hilo wanahitajika kurudisha ili na wengine waweze
kukopa.
Alisema wananchi wakope na waanzishe viwanda mbalimbali
vidogovidogo vya kusindika mazao, chelehani kushona nguo, kutengeneza batiki,
na wafanyakazi waende wakakope wajenge makadhi yao bora.
Alitaja shughuli fursa nyingine zilizopo mkoani humo ni
Pamoja na uvuvi, na aliwataka kubadilika kuacha
kufuga ngo’mbe kwa mazoe bali wafuge kisasa wawe wachache lakini wenye
tija.
Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa alisema kituo hicho kitasaidia kuwavutia wananchi kufanya shughuli
za biashara na ujasiriamali kwa vile ndani ya jengo hilo kutakuwa na taasisi
mbalimbali za kuwasaidia kuwapa huduma kwa haraka na kwa karibu kutimiza ndoto
zao.
“Katika jengo hili kutakuwa waratibu wa wilaya na mikoa wa
baraza, na taasisi nyingine kama benki ya NMB, CRDB, SIDO, TRA, BRELA,
TANTRADE, NIDA, TBS na Mfuko wa Self Microfinance,” alisema, Bi. Beng’i
Aliongeza kusema kwamba kituo hicho kinafanya baraza sasa
kuwa na vituo 20 nchi nzima na vinge
vinaendelea kujengwa na tayari vituo hivyo vimeeshatoa mikopo yenye thamani ya
shilingi bilioni 6.
Vilevile alisema hadi sasa watu 21852 wamesha tembelea vituo
hivyo na biashara zimesha rasimishwa.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigela amesema mafanikio
yanayopatikana katika mkoa huo
yanatokana na mshikamano ambao wameujenga na hiyo imekuwa ni nyenzo katika
utendaji na utoaji huduma bora kwa wananchi.
“Tutahakikisha tunafanya kazi ya kusawasaidi awananchi wetu
kulitumia jengo hilo,” dhamira yetu watu waweze kuwa matajiri kupitia shughuli
za biashara na ujasiriamali, aliongeza kusema.
Katika hafla hiyo ya uzinduzi wa jengo la kituo hicho pia Waziri Mkuu alifanya Mkutano na wananchi wa wilaya hiyo na kuzindua mwongozo wa Uratibu wa Uanzishaji na Usimamizi wa Vituo vya Uwezeshaji ili kuwezesha wananchi kushiriki katika Uchumi.
No comments