Breaking News

RAIS MWINYI ASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA MASHUJAA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameshiriki Maadhimisho ya siku ya  kumbukumbu ya mashujaa katika uwanja wa Mji wa Serikali,  Mtumba Jijini Dodoma tarehe 25 Julai 2024.

Mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan.

Viongozi mbalimbali wa Serikali kitaifa na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wameshiriki katika maadhimisho hayo.











No comments