Breaking News

WAFANYABIASHARA WAOMBA RUHUSA YA KUINGIA NCHINI NA DOLA KUANZIA 10,000

Mfanyabiashara Haidary Gulamali kwa niaba ya wafanya biashara wenzake akichangia jambo wakati wa kikao kilichofanyika Julai 12, 2024 Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Seleman Jafo.

................

Na Dotto Mwaibale

WAFANYABIASHARA wameiomba Serikali iwaruhusu kuingia nchini na dola za Marekani zenye thamani ya zaidi ya Sh. 10,000 wakati wakiingia na kutoka nchini kwa ajili ya shughuli zao za kibiashara jambo litakalosaidia kuinua uchumi wa nchi.

Ombi hilo limetolewa na Mfanyabiashara Haidary Gulamali kwa niaba ya wafanya biashara wenzake wakati wa kikao kilichofanyika Julai 12, 2024 Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Seleman Jafo.

“Mheshimiwa Waziri nchini kwetu hapa unapofika bandarini au Kiwanja vya ndege hairuhusiwi kuondoka na dola zaidi ya 10,000 kwani kiasi hicho cha fedha ndio kikomo cha kuwa nacho kwa mfanyabiashara au mtu yeyote atakaye kuwa akisafiri kutoka nchi ya nchi yetu, ”alisema Gulamali.

Gulamali alisema wakati kukiwa na zuio hilo kuna sheria kwa mtu yeyote atakaye kuwa anaingia nchini na dola zaidi ya 10,000 anazuiliwa.

“Sasa Mheshimiwa Waziri mtu ambaye anatoka Kongo, Zambia na nchi nyingine mbalimbali analeta nchini dola 10,000 au 20 uchumi wako si unakuwa na anapowekewa vikwazo hasilete zaidi ya dola hizo inaonesha sheria hiyo  inakuwa inapinga tusikusanye kodi,” alihoji Gulamali.

Gulamali alisema dola sio dawa ya kulevya ambapo aliomba kuwepo na sheria rafiki ya matumizi yake  kama ilivyo nchi nyingine ambazo mfanyabiashara anapokuwa dukani akinunua mahitaji yake anabadilishiwa papohapo. 

Mfanyabiashara Haidary Gulamali akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho.
 

No comments