WAZIRI MKUU ATOA WITO KWA TAASISI ZA DINI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia kwenye Kilele cha Mkutano wa Baraza la Maaskofu wa Makanisa ya Pentekoste Tanzania (CPCT), uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Biblia Miyuji jijini Dodoma.
..............................
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa taasisi zote za dini nchini
kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutoa mchango kwenye maendeleo ya
taifa.
Amesema kuwa taasisi za dini zina uwezo mkubwa wa kutoa huduma imara za
kiroho na kugusa maisha ya watu katika jamii na kuwaletea maendeleo ya kiuchumi
na kisiasa.
Ametoa wito huo leo (Ijumaa, Julai 19, 2024) kwenye Kilele cha Mkutano
wa Baraza la Maaskofu wa Makanisa ya
Pentekoste Tanzania (CPCT), uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Biblia Miyuji
jijini Dodoma.
“Tuna kila sababu ya kuyashukuru Makanisa kwa kuunga mkono juhudi
zinazofanywa na Serikali katika kuleta maendeleo ya wananchi kwa ujumla, yamekuwa
sehemu ya suluhisho katika changamoto za kijamii kama vile umaskini, elimu
duni, na matatizo ya kiafya”
“Nitumie fursa hii kusisitiza taasisi za dini kuendelea kuimarisha
ushirikiano na Serikali na kuendelea kuiishi kwa vitendo kaulimbiu yenu ya
Palipo na Umoja, Bwana huamuru baraka! Bwana huamuru baraka, palipo na Umoja”
Katika hatua nyingine Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali inathamini
uwepo na mchango wa taasisi za dini katika kuhubiri amani na utulivu nchini
“Siri ni ya haya yote ni sababu ya uwepo wa dini katika kuhubiri maadili,
mshikamano, upendo uvumilivu na kuwa wamoja, Serikali pekee tusingeweza”
Post Comment
No comments