ASAS MZALENDO ANAYECHOCHEA MAENDELEO MKOANI IRINGA
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (MNEC) Mkoa wa Iringa, Salim Abri Asas, akihutubia katika moja ya mikutano yake mkoani humo.
--------------------------------
Na Dotto Mwaibale
UZALENDO ni hali ya mtu kuipenda, kuithamini na kujitoa kwa ajili ya nchi na Mzalendo wa kweli wakati wote anaweka maslahi ya nchi na ya jamii mbele.
Uzalendo
unabeba dhana pana ikianzia asili, utamaduni, lugha, siasa, historia zote
zikifungwa kwenye dhana kuu ya utaifa.
Katika Taifa la Tanzania kumekuwepo na wazalendo wengi, baadhi wamekwisha tangulia mbele za haki akiwemo aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Tanzania Hayati Julius Kambarage Nyerere, Hayati Abeid Amani Karume, Hayati Rashid Mfaume Kawawa, Hayati Edward Moringe Sokoine, Hayati Edward Ngoyai Lowassa, Hayati Bibi Titi Mohamed na wengine wengi.
Leo napenda kumuongelea Salim Abri Asas ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (MNEC) Mkoa wa Iringa.
Kazi kubwa
anayoifanya Asas Mkoa wa Iringa katika kuimarisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) na
kujitolea kwenye masuala ya kijamii ni kubwa mno na inaonekana na kila mpenda
maendeleo mkoani humo na nchini kwa ujumla.
MNEC huyo amefanya mengi na anaendelea kuyafanya
bila ya kubagua makundi ya watu na hiyo ni kwa sababu ya hofu ya Mungu
aliyonayo.
Asas ambaye
ni mfanyabiashara mkubwa wa mazao yanayotokana na ng’ombe kupitia kampuni yake ya ASAS DAIRIES amekuwa akichagiza
maendeleo kwa makundi mbalimbali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na jumuiya zake.
Kuimarisha uhai
wa chama, Asas amefanya makubwa kwani kwa nyakati tofauti alitoa Sh.Milioni 13
kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Iringa.
Asas hakuishia
hapo, alitoa tena Sh. Milioni 5 kwa UWT Wilaya ya Kilolo kwa ajili ya kusaidia
ujenzi wa ukumbi.
Kutokana na moyo wake wa kizalendo, Asas ametoa msaada wa simu janja 36 kwa chama hicho Wilaya ya Mufindi alizosema zitumike kwa ajili ya usajili wa wanachama kidigitali katika kata zote.
Kwenye makundi ya kijamii Asas kupitia kampuni yake alitoa Sh.Milioni 100 kusaidia wafanyabiashara ndogondogo wa Iringa ili zitumike kujenga vibanda vya kufanyia biashara zao.
Hiyo ni baadhi ya michango kati ya mingi ambayo Asas amekuwa akiitoa kutokana na uzalendo alionao kwa Taifa lake la Tanzania.
Pamoja na kuwa kinara wa kuchagiza maendeleo ya wana Iringa na CCM
pia amekuwa mkali pale anapoona mambo hayaendi vizuri.
MNEC huyo amekuwa akikemea vitendo vya rushwa wakati wa chaguzi ambapo
kwa nyakati tofauti amekuwa akisema viongozi wanaopatikana kwa kununuliwa
hawawezi kuwatumikia wananchi.
Asas katika kuhimiza uimarishaji wa chama hicho alisema hakuna mtu
atakayetoka nje atakayefanya kazi hiyo
bali kitajengwa na wanachama wenyewe kwa kuwa wazalendona kujitoa.
Aidha, katika kuimarisha uhai wa chama mfanyabiashara huyo amekuwa
akifanya ziara za kikazi kwenye wilaya zote na kuhimiza suala la kuwatumikia
wananchi na kuwaletea maendeleo.
Mbali ya kazi kubwa anayoifanya pia amekuwa akishiriki katika
matukio ya kitaifa yanayofanyika mkoani humo yakiwemo ya mbio za Mwenge wa
Uhuru, uhamasishaji wa kutunza mazingira na mengine yanayofanana na hayo.
Kwa leo nakomea hapa, nakutakia kazi njema Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (MNEC) Mkoa wa Iringa, Salim Abri Asas ya kuwatumikia wana Iringa na Taifa kwa ujumla. Kazi Iendelee.Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (MNEC) Mkoa wa Iringa, Salim Abri Asas, akiweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Upendo.
No comments