Breaking News

WAZIRI MAVUNDE, MCHENGERWA KUSHUGHULIKIA TOZO ZA HALMASHAURI KWENYE MADINI

-Hii ni Kufuatia Changamoto za tozo za Halmashauri zilizowasilishwa na wachimbaji Morogoro

-Waziri Mavunde awapongeza Morogoro kuvuka lengo la makusanyo ya maduhuli

-Serikali kuongeza nguvu ya Utafiti Morogoro

-Wachimbaji wamshukuru Rais Samia kwa mashine za uchorongaji

Waziri wa  Madini Mh. Anthony Mavunde akizungumza katika kikao na wachimbaji wa Mkoa wa Morogoro.

................................

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

WAZI  wa Madini Mh. Anthony Mavunde amesema Wizara ya Madini imekubaliana na Ofisi ya Rais TAMISEMI kukutana na kutatua changamoto ya tozo zinazowekwa na Halmashauri kwa wachimbaji wa madini nchini.

Hayo yamesemwa jana Mkoani Morogoro na Waziri Mavunde wakati wa kikao cha wachimbaji wa Mkoa wa Morogoro kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji mkoani hapa.

“Nimesikiliza kwa umakini mkubwa kilio hichi cha tozo za Halmashauri na tozo nyinginezo kwa wachimbaji wadogo,kero hizi sio hapa tu zipo maeneo yote nchini.

Tunayo maelekezo ya Mh Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa kwamba Wizara hizi mbili zikutane kushughulikia suala hili.

Nataka niwahakikishe mimi na Mwenzangu Mh. Mohamed Mchengerwa tumekubaliana kwamba mara baada ya ziara ya Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassa mkoani Morogoro tutaitisha kikao cha pamoja ili kushughulikia suala hil”Alisema Mavunde.

Waziri Mavunde pia alichukua fursa hiyo kuwahakikishia wachimbaji wa Morogoro juu ya dhamira ya Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kuongeza nguvu kwenye eneo la Utafiti wa Madini ambapo na mkoa wa Morogoro pia utanufaika.

Mh Mavunde ameipongeza Ofisi ya Madini Mkoa wa Morogoro kwa kuvuka lengo la ukusanyaji maduhuli kufikia 4.9bn zaidi ya lengo lililowekwa la 4.2bn.

Akisoma Risala kwa niaba ya wachimbaji,Mwenyekiti wa Chama cha Wachimba Madini Mkoa wa Morogoro(MOREMA) Dkt. Omar Mzeru ameshukuru Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa kutoa mashine za uchorongaji kwa wachimbaji wadogo na kutumia fursa hiyo kumuomba Waziri wa Madini kushughulikia changamoto kubwa inayotokana na uwepo wa tozo nyingi zinatozwa na Halmashauri na Taasisi nyingine za serikali kwakuwa zimekuwa zikiwarudisha nyuma kimapato wachimbaji wadogo.

No comments